JESHI la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia Erick Julias (33) mkazi wa Miembeni wilayani Kilombero kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kufikia wa kiume mwenye umri wa miaka sita kwa kumnyofoa via vya uzazi pamoja na kukata viganja vyote viwili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP. Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea June Mosi mwaka huu Wilayani Kilombero Mkoani Morogo.
Kamanda Mkama amesema mtuhumiwa huyo kabla ya kufanya unyama huo alimtenganisha kichwa na kiwiliwili mtoto huyo.
Katika tukio jingine, Jovina Mwakiyee (33) mkazi wa kijiji cha Mang'ula A wilayani Kilombero anashikiliwa na Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kula njama na kumuua mume wake wa ndoa.
Kamanda Mkama amesema mwanamke huyo alipanga njama na Kisha kumuua mwanaume wake aliyeitwa Christian Tangaraza (39) ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Signal .
Kamanda Mkama amesema tukio hilo lilitokea usiku wa June Mosi mwaka huu ambapo marehemu aliuawa kwa kupigwa na kitu butu wakati akiwa amelala ndani ya nyumba yake.
Social Plugin