Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HALMASHAURI YA KISHAPU, MGODI WA MWADUI (WDL) WASAINI HATI YA MAKUBALIANO (MoU) KUTEKELEZA MIRADI YA CSR


Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakitia saini hati ya makubaliano ya utekelezaji miradi CSR na mgodi wa WDL kiasi cha Tsh.1,000,000,000/=  itakayotekeleza jumla ya miradi mbalimbali kumi na mbili (12) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 leo Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. PICHA na Sumai Salum


Na Sumai Salum - Kishapu

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga leo juni 27,2024 imesaini hati ya makubaliano (MoU) na mmiliki wa leseni ya madini Williamson Diamond Limited ya fedha za utekelezaji miradi ya CSR kiasi cha  Tsh.Bilion moja (1,000,000,000) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa jumla ya miradi 12.

Akizungumza kwenye Hafla fupi iliyofanyika leo Juni 27,2024  katika ukumbi wa Halmashauri kwa niaba ya Mkuu wa wilaya, Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu , Fatma Mohamed  ameipongeza kampuni hiyo ya madini WDL na amewataka kushirikiana na wataalamu wa halmashauri watekeleze kwa wakati huku wakizingatia ubora wa miradi.

"Ndugu zangu tunajivunia kuwa na wawekezaji kama ninyi katika Wilaya yetu kwani kwa kiasi hiki cha CSR kitasaidia jamii zote zinazozunguka Mgodi huu, hivyo nendeni mkae pamoja na wataalamu huku mkizingatia kasi ya utekelezaji miradi na si hivyo tu Bali zaidi sana ni kuangalia ubora wa miradi yenyewe", amesema  Fatma. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Bw. Emmanuel Johnson amesema hati hiyo ya makubaliano imezingatia sheria za madini sura ya 123 ya kanuni za mmiliki wa leseni za madini za mwaka 2023 na kutolewa mwongozo na TAMISEMI mwaka 2022 kwa mamlaka za serikali za mitaa kuhusu uwajibikaji kwa jamii kwa makampuni yenye leseni za madini.

Johnson amesema fedha hizo kutoka Williamson Diamonds Limited (WDL) zitasaidia kukuza kipato cha Halmashauri na jamii husika hivyo kupelekea kubadilisha maisha ya wananchi kwani watapata huduma bora na muhimu katika jamii wanazoishi.

"Kipekee tunaishukuru serikali ya Mhe. Samia Suluhu kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hata kupatikana kwa fedha na mipango ya kutekeleza miradi ya CSR kwa Halmashauri yetu hakika tutasimamia vyema fedha hizi kwa masilahi ya Halmashauri", ameongeza Mkurugenzi wa Kishapu

Aidha Meneja Mahusiano kutoka WDL Bw.Bernard Thomasi Mihayo ameipongeza Halmashauri hiyo na wako tayari kuhudumia jamii zinazowazunguka kwa kile wanachokipata.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Mhe. Willium Jijimya amewapongeza WDL na kuwasihi waendelee na uzalishaji kwa wingi ili fedha hizo wanazorudisha kwa jamii  ya mzunguko iongezeke zaidi.

Kwa upande wa mwakilishi wa madiwani wa mzunguko Mhe. Abdul Ngoromole amesema wakati wa utekelezwaji miradi hiyo ya maendeleo izingatie kuajiri mafundi hasa wa vijiji husika kwani itawasiaida kunyanyua vipato vya mtu mmoja mmoja na kuhudumia familia zao.

Fedha hizo za CSR zitatekeleza ujenzi wa zahanati ya Wizunza,Uanzishwaji ujenzi jengo la Mama na Mtoto kituo cha afya Maganzo,Ujenzi wa matundu Matano (5) ya vyote,Kichomea taka na ujenzi wa nyumba ya mtumishi 2 kwa 1 katika zahanati ya Mpumbula,Kuendeleza ujenzi wa jengo  la OPD na RCH kituo cha afya Idukilo,Kuanza ujenzi wa uzito wa waya mita 450 shule ya sekondari Mwadui Lohumbo,Ukamilishaji madarasa 2 na ofisi  shule shikizi Mwamala (Wishiteleja),Ujenzi wa ofisi ya Kata ya Mondo Miradi hiyo saba(7) itafanikishwa kwa 40% ya fedha hizo(400,000,000)

Ujenzi wa jengo la abiria katika stend ya basi Maganzo,Ujenzi wa maeneo ya maegesho ya gari za abiria stendi ya basi Maganzo,Kubiresha miundombinu ya mnada wa upili Kata ya Kishapu,Ujenzi wa mradi wa umwagiliaji Kijiji cha Iyenze na ufuatiliaji na usimamizi wa Miradi ya CSR 10% na miradi hiyo pia itakamilishwa mwa 60% ya fedha hizo(600,000,000).
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakitia saini hati ya makubaliano ya utekelezaji miradi CSR na mgodi wa WDL kiasi cha Tsh.1,000,000,000 itakayotekeleza jumla ya miradi mbalimbali kumi na mbili (12) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Leo Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. PICHA na Sumai Salum
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ,Emmanuel Johnson (suti ya kijivu) na Meneja Mahusiano WDL Bernard Thomas Mihayo (shati ya bluu) Leo Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri wakikabidhiana hati waliyotia saini makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi cha Bilioni moja itakayotekeleza jumla ya miradi 12.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambaye ni Katibu Tawala Wilaya hiyo na mgeni rasmi Fatma Mohamed akizungumza kwenye tukio la utiaji saini kati ya Kishapu DC  na WDL fedha za CSR Tsh.1,000,000,000 Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambaye ni Katibu Tawala Wilaya hiyo na mgeni rasmi Fatma Mohamed akizungumza kwenye tukio la utiaji saini kati ya Kishapu DC  na WDL fedha za CSR Tsh.1,000,000,000 Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Emmanuel Johnson akisoma taarifa ya utiaji saini hati ya makubaliano ya utekelezaji miradi ya CSR na mmiliki wa leseni ya madini WDL juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo kiasi cha Tsh.1,000,000,000 fedha itakayotekeleza miradi kumi na mbili (12).

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga akizungumza Leo juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo katika zoezi la utiaji saini kati ya KDC na WDL hati ya makubaliano ya utekelezaji miradi CSR kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi  Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Francis Mashenji akizungumza katika utiaji saini hati ya makubaliano (MoU) ya utekelezaji miradi ya CSR Leo juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo kiasi cha Tsh.1,000,000,000 itakayotekeleza miradi mbalimbali kumi na mbili (12).

Mwakilishi wa Madiwani wa Mzunguko na Diwani wa Kata ya Songwa Wilayani Kishapu Mhe. Abdul Ngoromole akizungumza kwenye hafula ya utiaji saini hati ya makubaliano ya utekelezaji miradi ya CSR kati ya Halmashauri hiyo na Mmiliki wa mgodi wa WIlliamson Diamond Limited Juni 27,2024
Maafisa kutoka kampuni ya madini ya WDL kushoto ni Bi.Hilda George Hizza (Afisa malalamiko WDL) katikati ni Bernard Thomas Mihayo (Meneja Mahusiano WDL) na kulia ni  Bi.Sylvia Leonidas Mulongo (Mwanasheria WDL) katika tukio la utiaji saini Tsh.Billion Moja( 1,000,000,000) ya CSR na Halmashauri ya wilaya Kishapu Mkoani Shinyanga juni 27,2024.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com