RC KIHONGOSI AKARIBISHWA RASMI NA WAGANGA WATIBA ASILI SIMIYU, APEWA JINA "MASANJA"


Bariadi,

Waganga wa tiba mbadala na  na tiba asili Mkoani Simiyu wamemkaribisha rasmi Mkoani humo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenan Laban Kihongosi.

Mhe.Kihongosi amepewa jina "Masanja"katika hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Makuti iliyoko  Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Wataalamu hao wa tiba asili na tiba mbadala, Mhe.Kihongosi amewashukuru kwa mapokezi mazuri na amewaahidi ushirikiano wa kutosha katika kipindi cha utekelezaji wa majukumu makubwa aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya  kuuongoza Mkoa wa Simiyu.

Amewataka Waganga hao kujiepusha na Mila potofu ikiwemo ramli chonganishi  zinazohatarisha maisha ya baadhi ya Watu hususani wa makundi ya wenye uhitaji maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi almaarufu Albino.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe.Simon Peter Simalenga akimkaribisha Mkuu wa  Mkoa kuzungumza na Wataalamu hao amesema  Wilaya ya Bariadi na Mkoa kwa ujumla unatambua jitihada na ushirikiano mkubwa wa Waganga wa tiba Asili katika uhamasishaji na uchangiaji nguvu kazi katika Miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amemuambia Mkuu wa Mkoa Mhe.Kihongosi kuwa Waganga wa tiba Asili Mkoani Simiyu wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia kwa hali na mali kufanikisha shughuli mbalimbali za Kiserikali akitolea mfano ujenzi wa Madarasa katika Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Simiyu.

Kwa upande wao Waganga wa tiba asili na tiba mbadala Mkoani Simiyu wamemhakikishia Mhe.Kihongosi kuwa watandelea kushirikiana vyema na  Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

John Mganga,
SIMIYU RS 
28 Juni 2024.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post