Afisa mwandamizi wa Huduma na Elimu kwa mlipakodi kutoka TRA Mkoa wa Morogoro Emmaculate Chaggu akikemea suala la wafanyabiashara kujaribu kuvunja sheria za kodi kwa kulazimisha wanunuzi kuongeza malipo pindi wanapotaka risiti za kielektroniki baada ya kupata huduma. (Picha zote na Christina Cosmas, Morogoro)
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo Ruth Eliud akiishukuru Taasisi ya Suyoo kwa kuwakutanisha na wadau wa biashara ambao anaamini watamuinua kutoka hatua moja hadi nyingine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya vijana Resolution Group James Suka akizungumzia umuhimu wa warsha hiyo kwa wanafunzi na wadau wa masomo ya biashara katika warsha waliyoiandaa ili kukuza taaluma za vijana nchini.
Na Christina Cosmas, Morogoro
MAMLAKA ya Mapato (TRA) mkoa wa Morogoro imekemea kitendo cha wafanyabiashara kujenga tabia ya kudai kuongezewa hela ndipo watoe risiti za kielektroniki bali wampatie mteja risiti anayohitaji kulingana na huduma aliyopata.
Afisa mwandamizi wa Huduma na Elimu kwa mlipakodi kutoka TRA Mkoa wa Morogoro Emmaculate Chaggu amesema hayo wakati wataalamu na wanafunzi wa fani za biashara 300 walipokutanishwa ili kuboresha mahusiano.
Chaggu anawataka wafanyabiashara kutoa risiti kwa kutumia mashine za EFD kama sheria inavyowataka ili kuiingizia serikali mapato yatakayosadia kuboresha shughuli za maendeleo na kujiepusha na kupata adhabu ikiwemo kutozwa faini.
“ malalamiko yapo kwa baadhi ya wateja kuwa muuzaji akidaiwa risiti yeye nae anamdai mnunuzi amuongezee hela ili aweze kumpa risiti halali anayoitaka ya EFD, tunasisitiza wanunuzi msikubali kufanyiwa hivyo toeni taarifa mapema TRA itawashughukia" anasema
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya vijana inayohusika na kutoa elimu na mitihani ya bodi (Suyoo vijana Resolution Group) James Suka anasema wameona upo umuhimu mkubwa wa kuwakutanisha wanafunzi hao na wataalamu mbalimbali wa fani ya biashara ili kuboresha elimu zao.
Anasema pia kupitia mada mbalimbali zinazotolewa anaamini wanafunzi hao watawiva na kuwa tayari kibiashara hapo baadae.
Mmoja wa washiriki Ruth Eliud aliishukuru Suyoo kwa elimu wanayoendelea kuwapatia huku wakiwakutanisha na wadau mbalimbali wa biashara ambapo anaimani wanaweza kuwasaidia kufikia malengo yao
MWISHO….
Social Plugin