Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Richard Mabala - Picha na Kadama Malunde
Na Marco Maduhu, Dar es salaam
TAASISI ya Vyombo vya habari kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN), wametoa Tuzo za heshima kwa Vinara wa uhuru wa kujieleza.
Vinara waliopewa Tuzo hizo ni Maxence Melo, Ndimara Ntengabwage, Richard Mabala, Ally Masoud, Prof Issa Shivji, Salma Said na Twaha Ulimwengu.
Tuzo hizo zimetolewa leo Juni 1,2024 na Mgeni Rasmi Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ikiwa ni siku ya Pili ya Kongamano la Kufanya Tathmini ya Hali ya uhuru wa Kujieleza, Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Wana Habari mwaka 2024 lililoandaliwa na MISA TAN Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizabeth Riziki amesema Tuzo hizo wamezitoa kwa Vinara wa Uhuru wa kujieleza na zitakuwa endelevu.
"Tulichagua watu wachache wa kuanza nao ambao wamekuwa wachechemuzi na vinara wa uhuru wa kujieleza bila kuvuruga amani wale kukiuka sheria za nchi," amesema Riziki.
Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN Wakili James Marenga, amesema Tuzo hizo ni mwanzo tu na kwamba waliona ni vyema kuwapatia shukrani hizo wakiwa bado hai,kutokana na mchango wao mkubwa katika Tasnia ya habari na kuchechemua uhuru wa kujieleza.
Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi ameipongeza MISA-TAN kwa kutoa Tuzo hizo na kuheshimu watu walio na mchango suala la uhuru wa kujieleza.
Amesema Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kulinda Uhuru wa kujieleza na hata alipoingia Madarakani mwaka 2021,alianza kufungulia Magazeti manne ambayo yalikuwa yamefungiwa, pamoja na kutoa maelekezo ya Sera ya habari na utangazaji na huduma ya habari kufanyiwa marekebisho ili kuwepo na uhuru wa habari.
"Nafurahi kufanya kazi nikiwa na Amanj kwa nchi ambayo ina heshimu Uhuru wa habari"amesema Matinyi.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwenye Kongamano la Kufanya Tathmini ya Hali ya Kujieleza, Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Wana Habari Jijini Dar es salaam - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwenye Kongamano la Kufanya Tathmini ya Hali ya Kujieleza, Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Wana Habari Jijini Dar es salaam
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) , Wakili James Marenga akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) , Wakili James Marenga akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) , Elizabeth Riziki akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi (kulia) akikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa Maxence Mello, ndugu Kadama Malunde
Picha Hapa chini ni : Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akikabidhi tuzo kwa wawakilishi wa washindi wa tuzo
Social Plugin