ADHABU MBADALA KUPUNGUZA MSONGAMANO GEREZANI

 

Na Dotto Kwilasa,Manyara

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema Serikali imefanikiwa kupunguza msongamano katika Magereza mbalimbali nchini mara baada ya kuanza kutekeleza adhabu mbadala kwa wafungwa wanaotumikia adhabu za nje ya Magereza ambapo takriban wafungwa 2000 kila siku wanatumikia adhabu za nje

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Uangalizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Nsanze mkoani Manyara wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa wadau wa haki jinai iliyoandaliwa na Wizara hiyo, kwa kuwashirikisha wadau wa idara ya Mahakama, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Huduma za Uangalizi wa Polisi, Magereza pamoja na Ustawi wa Jamii

“Mkusanyiko wa leo kwa wadau wa Haki Jinai waliokusanyika hapa Manyara ni pamoja na kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Haki Jinai ya kuboresha Taasisi ya Haki Jinai hapa nchini lengo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Tume hiyo ni kufanya maboresho ya Haki Jinai katika kuongeza weledi ili kutoa huduma bora kwa watu wote" alisema
Hata hivyo, ametoa wito kwa Mahakama nchini kuhakikisha kwamba utekelezaji wa sheria hiyo inatekelezwa kwa wafungwa wanaofaa na walioanishwa katika sheria za nchi, kupewa adhabu mbadala ya kuitumikia jamii, kwa kufanya kazi bila malipo ili kupunguza gharama za uendeshaji ikiwemo kuhudumia wafungwa vyakula na mahitaji mengineyo

Amesema pamoja na mambo mengine malengo makubwa ya adhabu hizi ni urekebishaji wa tabia kama ushauri nasaa kwa wafungwa walioathirika na madawa ya kulevya ambapo hupata fursa ya kupelekwa Soba House na kupata matibabu, huku waathiriwa wa Virusi Vya Ukimwi(VVU) wakiunganishwa na vituo vinavyotoa huduma za ARV

Ikumbukwe kuwa Idara hiyo inatekeleza sheria zinazotoa huduma ambayo ni sheria ya huduma kwa jamii Sura 291, Sheria ya uangalizi kwa wahalifu Sura 247, Sheria ambazo kwa ujumla wake zinataka wafungwa waliokutwa na hatia na waliofungwa kifungo kisichozidi miaka mitatu kutumikia adhabu zao ndani ya jamii kwa kufanya kazi bila malipo, katika Taasisi za Umma ikiwemo Hospitali, Mahakama na Taasisi zinginezo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post