KASHWASA BINGWA MASHINDANO YA ATAWAS MAJI CUP LEAGUE LAKE ZONE 3, 2024


Ligi ya ATAWAS Maji CUP Lake Zone 3, imetamatika huku Timu Tano za Mpira wa Miguu Kanda ya Ziwa namba Tatu zikifuzu kushiriki Ligi hiyo Kitaifa, ambapo Timu Nne ni kutoka Mamlaka za Maji,na Timu Moja ya Jamii. 

Ligi hiyo inashirikisha Timu za Mamlaka za Maji kutoka Kanda 10 pamoja na Timu za Jamii, ambapo kuanzia Jana hadi leo yenye kauli Mbiu isemayo 'Thamani ya Maji kwa Uhai na Maendeleo' ilikuwa ni Michezo kutoka Kanda ya Ziwa Namba 3 ili kupata Timu Nne za Mamlaka za Maji na Timu Moja ya Jamii ambazo zitakwenda kushiriki michezo hiyo Dodoma Septemba mwaka huu 2024 pamoja na Timu mbili za Mpira wa Pete ili kupata mshindi katika Timu 32 kutoka Kanda zingine.


Mtendaji Mkuu wa ATAWAS Costantino Chiwaligo, akitangaza Matokeo amesema katika Mashindano hayo zilipaswa kushiriki Timu Saba za Mamlaka za Maji, lakini ambazo zimeshiriki Ligi hiyo ni Timu Nne, huku Timu Tatu zikishindwa kushiriki, na hivyo kusababisha Timu Nne kufuzu Moja kwa Moja kwenda Jijini Dodoma.

 

Amezitaja Timu za Mamlaka za Maji ambazo zimefunzu kwenda Dodoma, kuwa ni KASHWASA, SHUWASA, MAUWASA na MWANHUZI,huku Timu za Jamii ni Polisi Jamii ambayo itashiriki mashindano hayo Dodoma.

 

“Timu ambazo hazijashiriki Ligi hii ya Maji Cup kwa upande wa Kanda ya Ziwa namba Tatu ni KUWASA,KISHAPU na BARIADI, na Timu za Pete ambazo zitakwenda Dodoma ni SHUWASA na Mwanhuzi,”amesema Chiwaligo.


Aidha, ametaja Mshindi wa Jumla katika Mashindano hayo kwa upande wa Kanda ya Ziwa namba 3, kuwa ni KASHWASA, Wa pili Polisi Jamii, Wa tatu Ibadhi na Wanne SHUWASA.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, amewapongeza washindi wote katika michuano hiyo, na kuwataka wajiandae vizuri kwa sababu Dodoma kutakuwa na Ushindani mkubwa.

 

Katika uhitimishaji wa Ligi hiyo Timu za Jamii zilipewa Zawadi ya Mipira,ambazo ni Ibadhi,Polisi Jamii,na Shinyanga Veterani Academic.


Lengo la Ligi hiyo ya ATAWAS Maji Cup ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa Jamii, juu ya kutunza vyanzo vya Maji,Miundombinu ya maji na kuzuia upotevu wa Maji.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akikabidhi zawadi kwa washindi wa pili katika mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akikabidhi zawadi mara baada ya  mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akikabidhi zawadi mara baada ya  mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akikabidhi zawadi mara baada ya  mashindano hayo.

 Mtendaji Mkuu wa ATAWAS Costantino Chiwaligo akizungumza wakati wa mashindano hayo.


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza wakati wa mashindano hayo.







Shirika la msalaba mwekundu wakitekeleza majukumu yao wakati mechi ikiendelea uwanjani hapo .

Mchezo ukiendelea.

Mchezaji kutoka timu ya KASHWASA Kanjo Werner wakati fainal ikiendelea.

Mchezo ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post