Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Phaustine Kasike leo amemtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Mha. Ladislaus Matindi na kufanya mazungumzo kuhusu fursa za usafiri wa anga kati ya Tanzania na Msumbiji. Viongozi hao wamekubaliana kuangalia uwezekano wa ATCL kutumia fursa hizo ili kutanua wigo wa biashara. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya ATCL.
Social Plugin