Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BARAZA JIPYA NACONGO LAANZA KAZI RASMI

Na Zena Mohamed

BARAZA jipya la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO)laanza kazi rasmi baada ya kuzinduliwa jana, Juni 26,2024 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt.Dorothy Gwajima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini,Dodoma leo Juni 27,2024, kuhusu vipaumbele vya Baraza hilo atika kipindi cha kutekeleza majukumu yao kwa mwaka 2024 hadi ifikapo mwaka 2027 

Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Jasper Makala amesema kuwa wamejipanga kurekebisha mapungufu yote ya Baraza lilopita huku akitaja vipaumbele vya Baraza hilo jipya.

Ambapo amesema kuwa Baraza la mashirika yasiyo ya kiserikali limejipanga kusaidia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika nyaja mbalimbali ikiwemo kuzijengea uwezo mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kitaaasisi na kiutendaji

Kusaidia mashirika kuzingatia sheria na taratibu za nchi, kuimarisha mashirikiano kati ya serikali na mashirika yasiyokuwa yakiserikali,kuimarisha Ushiriki wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika kuchangia katika Dira za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC) Jumuiya ya Umoja wa Africa (AU) na Malengo endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa (UN).

Pamoja na kupashana taarifa mbali mbali zitakazo chagiza uwepo wa fursa na kuongeza ujuzi na weledi wa mashirika na umma kiujumla.

"Kama mnavofahamu, kama taifa kuna mikakati na mipango ambayo tunajiwekea kama nchi, na kushirikiana katika kuleta maendeleo ya Taifa,"amesema.

Makala amesema kuwa wao kama Baraza wamejipanga kuongeza juhudi katika kutekeleza mipango ya Taifa kama Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, mikakati mbali mbali katika kuwa na Tanzania Bora kwa watanzania wote.

"Dira ya maendeleo – 2050,sisi wana AZAKI tumeanza kutoa mchango wetu katika kuhakikisha Dira hiyo inazingatia suala zima la maendeleo jumuishi, hususani ushiriki wa makundi maalum katika shughuli za kiuchumi na huduma za jamii unapewa kipaumbele katika utekelezaji wa afua mbalimbali za serikali na wadau wake,"amesema Makala.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com