Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BILIONI 30 KUIMARISHA HUDUMA ZA WATOTO WACHANGA KATIKA HOSPITALI 100 NCHINI

 

Na WAF-Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya imepanga kutumia shilingi bilioni 30 kuimarisha huduma za watoto wachanga kwenye hospitali 100 nchini kwa kujenga wodi maalum (NCU) za Watoto wachanga, Watoto njiti na ununuzi na usambazaji wa vifaa tiba ikiwemo mashine za kuwasaidia Watoto wachanga njiti kupumua.

Hayo yamebainisha na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Bungeni jijini Dodoma Juni 03,2024  wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu katika bunge la 12, mkutano wa 15 na kikao cha 39

Dkt. Mollel amesema kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali ilipeleka vifaa vya kusaidia Watoto njiti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya 241 vyenye jumla ya thamani ya bilioni 2.6 hadi kufikia machi 2024.

Wakati huo huo Dkt. Mollel ameweka msisitizo kuwa, Serikali kupitia Sera ya Afya ya Mwaka 2007 imeweka utaratibu wa Wagonjwa wote wa dharura kupatiwa huduma za Afya za dharura kwanza pasipo kikwazo cha kulipia huduma hadi atakapo tatuliwa changamoto za kiafya zinazo mkabili.

“Natoa wito kwa waganga wakuu wa vituo vyote kuhakikisha wagonjwa wa dharula wanapata huduma wanazostahili kwanza ili kuokoa Maisha yao na taratibu nyingine zifuate baada ya kuwa wamehudumiwa”, ameelekeza Dkt. Mollel.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com