Na Mwandishi wetu _ Malunde 1 blog
Waziri wa Fedha nchini Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameshuhudia hafla ya utiaji saini Kandarasi ya ujenzi wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria kwenye halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hafla hiyo imefanyika leo Juni 02, 2024 katika Kijiji cha UIowa kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama ukishuhudiwa pia na Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso pamoja na viongozi mbalimbali.
Akisoma taarifa ya utekelezajinwa mradi huo Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo ameeleza gharama za utekelezaji wa mradi huo pamoja na manuafaa pindi utakapo kamilika.
"Mradi huu unatarajiwa kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 44 na kutekelezwa kwa muda wa miezi 22 ambapo leo tutakwenda kusaini kandarasi kwa ajili ya utekelezaji, kukamilika kwa mradi huu kutachochea maendeleo kwa wananchi wa Ushetu kwa kuondokana adha ya kutafuta maji ambapo zaidi ya watu laki 1 watafikiwa na huduma hii ya maji kutoka ziwa Victoria", amesema Mhandisi Kivegalo.
"Mradi huu utahusisha ujenzi wa mfumo wa kutibu maji, ujenzi wa vituo 33 vya kuchotea maji, mfumo wa kusambaza maji, usimikaji mifumo inayoweza kutoa huduma lakini pia ujenzi wa jengo la ofisi kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi, mradi huu utaanza mara baada ya zoezi la utiaji saini kukamilika", ameongeza Mhandisi Kivegalo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani amesema ujio wa mradi huo ni historia kwa wakazi wa Ushetu kutokana na changamoto ya maji iliyodumu kwa muda mrefu.
"Wananchi hawa wamesubiri mradi huu kwa muda mrefu lakini leo historia imeandikwa kwao, nikumpongeze Mheshimiwa Waziri wa Maji pamoja na Waziri wa fedha kwa kufanikisha mradi huu lakini pia tuendelee kumuombea Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu, niwaombe wakandarasi hawa watoe kipaumbele kwa vijana wetu katika ajira pindi mradi huu utakapoanza kutekelezwa", amesema Cherehani.
Kwa upande wake Waziri wa Maji nchini Mheshimiwa Juma Aweso amesema Wizara ya Maji itaendelea kutoa kipaumbele kwenye maeneo ambayo bado yana changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa kutoa kipaumbele kwenye sehemu zenye dharura, na kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti kwenye sekta ya maji nchini ili kuongeza mtandao wa maji kwa wananchi,
Akizungumza mara baada ya zoezi la utiaji saini kukamilika Waziri wa fedha nchini Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amewasihi wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo hata baada ya kukamilika ili idumu na ikawe na manufaa kwa vizazi na vizazi.
"Itoshe kusema salamu za Dkt. Samia Suluhu Hassan zimefika kwa wananchi wa jimbo la Ushetu, Bilioni 44.2 zilitotolewa hapa inaonesha kujali matatizo na changamoto za watu wa eneo hili, ambapo zaidi ya vijiji 50 vitafikiwa na huduma hii ya maji safi na salama, ndio maana leo hii nimefika hapa kushuhudia zoezi hili la utiaji saini",
"Kuhusu changamoto ya barabara pamoja na ujenzi wa kituo cha afya kwenye kata hii kama wizara ya fedha tumelipokea tutakwenda kulifanyia kazi, mara baada ya kukamilika kwa mradi huu niwasihi wananchi tukawe walinzi wa miundombinu hii ili ikawe na manufaa na kuduma kwa muda mrefu", ameongeza Mheshimiwa Mwigulu.
Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utiaji saini.
Zoezi la utiaji saini likiendelea.
Zoezi la utiaji saini likiendelea.
Zoezi la utiaji saini likiendelea.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Shinyanga Dk. Christina Mzava
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utiaji saini.
Waziri wa maji nchini Mheshimiwa Jumaa Aweso akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utiaji saini.
Waziri wa fedha nchini Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi hilo la utiaji saini mradi wa maji ya ziwa Victoria.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi hilo la utiaji saini mradi wa maji ya ziwa Victoria.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia zoezi hilo la utiaji saini mradi wa maji ya ziwa victoria.