Na Hadija Bagasha Tanga
Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania, chini ya ufadhili wa NORAD,wamekabidhi Boti ya kisasa kwaajili ya kufanya doria kulinda rasilimali za bahari na pwani katika Muqtada wa kudhibiti uvuvi haramu.
Boti hiyo ni yapili kutolewa wilayani Mkinga kwa kamati ya uhifadhi wa Bahari ya eneo moja la uvuvi( CFMA- collaborative Fisheries management area) ya Boma Mahandakini yenye vijiji tisa.
Kutolewa kwa boti hi litasaidia kuongeza wigo wa doria za ulinzi kwa Vijiji zaidi ya 9 vya kata za Boma na Moa.
Akikabidhi Boti hiyo yenye thamani ya takribani shilingi milioni 40 kwa ajili ya doria pamoja na vifaa vyake kamili kama mashine,vifaa vya mawasiliano zikiwemo Simu za mkononi na vinasa sauti za redio, vifaa vya kujiokoa,vifaa vya huduma ya mwanzo pamoja na
darubini .
Mradi huo unatajwa kwenda kuwanufaisha Wakazi wa kata za Boma na Moa wilayani Mkinga.
Mratibu wa Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania Mkoa wa Tanga, Ahmad Salim Omar amesema,
lengo la kutoa Boti hiyo ni kuwasaidia kamati kwaajili ya kuendesha doria zenye tija Baharini ili kudhibiti uvuvi haramu na hii inakwenda sambamba na kauli mbiu ya Mwambao ya Afya ya Bahari ni Utajiri wa jamii_ 'Ocean health is Community wealth'.
"Boti hii ni ya kisasa tunaikabidhi rasmi kwenu Wanaboma mahandakini ikiwa na Vifaa vyake kamili kwwvajili ya doria. Botii hii baada yaa kufika tulitaka ianze kazi , hatukutaka kulala na kwa kipindi cha miezi miwili imeweza kukamata vyombo mbalimbali vya baruti na milipuko , wavuvi haramu na wale wasio na leseni za uvuvi, "amesema
"Kuna wavuvi haramu ambao wameshakamatwa na wamelipa faini takribani milioni 5 hii kwa maana nyingine imeisaadia Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuongeza mapato yake ambayo ni muhimu katika shughulii za uhifadhi na usimamizi wa rasilimali za bahari" Aliongeza Ahmad Omar
Aliwataka Wakazi wanaoishi Mwambao wa Bahari Kutunza rasilimali z a ahari ili kuongeza uzarishaji wa Samaki na kipato,
"Lengo letu kama Shirika ni kunga jitihada za serikali katika usimamizi endelevu wa raslimali za bahari na ku uwasaidia wavuvi kuongeza kipato chao, tukiamini uvuvi salama na rafiki wa mazibgira utapelekea kuimarisha Mazalia ya samaki ambapo kiwangs chs upatikanaji ws ssmakii kuongezeka.
"Naomba mtunze rasilimali za Bahari, lakini pia naomba matumizi sahihi ya boti hii na utunzaji li ili kifanye kazi iliyokusudiwa na Shirika", amesisitiza Omar
kwaupande wake, Katibu tawala Wilaya ya Mkinga Palangyo Abdul, amelishukuru Shirika hilo kwa msaada huo wa kusaidia juhudi za Kutunza rasilimali za Bahari,
"Tunawashukuru sana Mwambao Coastal Community Network Tanzania pamoja na Wadau wa NORAD,kwa juhudi zenu za kusaidia mapambano dhidi uvuvi haramu,lakini pia mnaisaidia Serikali, niwaombe Wananchi wenzangu msiwaangushe Wadau hawa, tunataka tuone juhudi zao zinaleta matokeo chanya kwa Jamii yetu,tunzeni rasilimali Bahari ili muongeze kipato chenu",ameongeza Palangyo.
Social Plugin