"ZIGO" LA MIAKA KUMI LAMUELEMEA MTENDAJI WA MTAA WA MTAMBANI, MARIA SAMWEL,ALITUA KWA WANANCHI

OFISA Mtendaji wa Mtaa wa Mtambani, Maria Samwel akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Mtaa huo, katika Mwaka Mmoja. 

Wananchi wakimsikiliza mkandarasi wa taka akitoa maelezo yake

**

"ZIGO" la miaka Kumi limemuelemea Mtendaji wa Mtaa wa Mtambani, Kata ya Tabata jijini Dar es Salaam, Maria Samwel, amelitua kwa wananchi mkutanoni.

Mmoja wa wakazi wa Mtaa huo anapopata nafasi ya kuuliza swali, anaomba kujua kwanini hawakusomewa mapato na matumizi ya mtaa wao?

Samwel anasema amepata wadhifa huo kwa takriban Mwaka Mmoja mpaka wakati huo, (Juni 17, 2024) na kwamba alikuta hali isiyoeleweka wala kuelezeka kuhusu eneo la mapato na matumizi.

"Wajumbe wa Kamati zinazotakiwa kutekeleza majukumu yake kwa namna ya kuwezesha ofisi kuweza kuandaa taarifa ya mapato na matumizi, hawakuwa wakifanya hivyo kwa miaka yote ambayo wamekuwa madarakani," anasema Samwel.


Serikali ya Mtaa huo imekuwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti, Brigitha Nchimbi kwa Miaka Kumi sasa, ambaye aliueleza  mkutano huo kwamba hali hiyo ilitokana na kutokuwa na Ofisa Mtendaji kwa kipindi chote hicho, kwamba kwa ujio wa Samwel, watarajie mabadiliko katika eneo hilo.

Kwa upande wake mtendaji huyo alibainisha kwamba anaendelea kurekebisha kasoro alizozikuta na kuahidi ataanza kutoa taarifa za mapato na matumizi katika vikao vitakavyofuata, kwa mujibu wa taratibu.

Hayo yamejiri Jumatatu wiki hii, (Juni 17 Mwaka huu) kwenye mkutano wa mtaa uliofanyika kwenye eneo la Ashery, jirani na ofisi za serikali ya Mtaa wa Mtambani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post