Na Hadija Bagasha Tanga.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi 'CCM' Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman ameendelea kusisitiza viongozi kutekeleza agizo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alilolitoa hivi karibuni kwa wakuu wa wilaya na mikoa kuwataka viongozi na watendaji wote kuacha kutumia mabavu kwa wananchi wanaowaongoza.
Kauli hiyo ameitoa wilayani Handeni katika ziara yake alipofika kukagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kibaya kata ya Misima ambapo licha ya kutoa Milion 4 tangu February 2024 kwaajili ya ununuzi wa Tofali umeshindwa kuanza kwa wakati kutokana na mvutano baina ya wananchi huku wakidai kutokushirikishwa kwenye miradi pamoja na kutishiwa kupelekwa Polisi na viongozi wao pale wanapohoji kinachoendelea.
Rajabu aliwataka viongozi hao wakae pamoja na wananchi wa kijiji hicho cha Kibaya ili kuondoa tofauti zilizopo ambapo kati ya vitongoji vinne vilivyopo ni wananchi wa vitongoji viwili pekee ndio wanaoshiriki katika ujenzi wa zahanati hiyo.
" Viongozi wenye kutumia ubabe Mheshimiwa Rais hataki kuwaona kabisa viongozi hao , ubabe wa nini ? wewe unawaongoza watu wenye akili zao timamu na maarifa kama wanakosea wajibu wako kama kiongozi unapoona wananchi wanalalamika ujue kuna tatizo sio bure " alisema Rajabu.
"Kijiji hiki kina vitongoji vinne zahanati hii ni ya vitongoji vyote haiwezekani wananchi wa vitongoji fulani hawashiriki wanashughulika wengine lazima wananchi wa vitongoji vyote nao washiriki katika mradi huu kutoa nguvu zao,viongozi niwaelekeze twendeni tukakae nao kwanini hawashiriki kisha baada ya hapo tuondoe tofauti hizo,kuhakikisha kwamba mgogoro huu unamalizika lakini mradi huu lazima uendelee kama tulivyokusudiwa ili kuwapunguzia na kuwaondolea wananchi adha hizi za kukosa huduma ya afya karibu"
"Nina timu yangu inayopita mkoa mzima huu wa Tanga miradi yote ya serikali tunapita kuangalia mambo yanaendaje ni kweli wananchi hawa hawashirikishwi katika mradi huu na katika miradi mingine , katika maelekezo ninayoyatoa kuanzia sasa lazima wananchi hawa washirikishwe hatua moja baada ya nyingine lazima wananchi wote washiriki kutoa nguvu zao katika mradi huu"
Awali akizungumza mmoja wa wananchi wa kijiji hicho cha Kibaya Hamza Mazimu alisema kuwa eneo hilo hakuna huduma za afya karibu,hivyo inawabidi kutembea kilomita saba,sawa na kilomita 14 kwenda na kurudi kata ya jirani kufuata huduma ya afya.
Alisema kumekuwa na changamoto ya kutokushirikishwa kwa wananchi wa Kijiji hicho katika utekelezaji wa miradi mbalimbali hali ambayo imekuwa ikichangia mvutano baina yaona viongozi kocha ya kukosa huduma za afya kwa kipindi cha muda mrefu hatua ambayo imekuwa ikiwafanya kutembea umbali wa kilomota 7 kufuata huduma katika kata za jirani.
"Wananchi wa Kijiji Cha Kibaya walichanga nauli zao kwenda mpaka ofisi ya Mkurugenzi kudai Zahanati kwa sababu wakina mama wanateseka Sana, tunachifanywa Sasa hivi ni kuwajibishwa na sio kushirikishwa hatuwezi kupelekea hivyo na ukizingumza unaweza kupelekea Polisi kwaajili ya kudai haki za wanakijiji lakini kama tutashirikiahwa tutachangia mpaka kuhakikisha Zahanati inasimama" alisema Mazimu
"Hapa inatubidi kutembea kilo saba kwenda kata ya jirani kufuata huduma za afya,wanawake ndio wanateseka zaidi kwa kutembea umbali mrefu,hivyo ujenzi wa zahanati hii ni muhimu sana kwetu ila mtendaji wa kijiji amekuwa ni kikwazo kwetu kufanikisha ujenzi huu", aliongeza.
Zahanati hiyo yakijiji cha Kibaya inayojengwa kwa nguvu za wananchi tayari Mwenyekiti chama Cha Mapinduzi alichangaia kiasi Cha Milion 5.500,000 kwaajili ya ununuzi wa Tofali , ujenzi wa msingi pamoja na ununuzi wa mchanga ambapo tayari ujenzi huo umeshaanza.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando amekiri kuwepo mgogoro huo wa mvutano baina ya wananchi wa Kijiji hicho waliokuwa wakizozana juu ya ujenzi wa Zahanati tangu Februari mwaka huu ambapo tayari ofisi yake kwa kushiriki na chama waliutatua na hatimaye kufikia makubaliano ya kuanza kwa ujenzi.
"Mgogoro huu tunaufahamu alikuja afisa tarafa tukaongea nao likapatikana suluhisho baada ya hapo uliotokea mvutano mwingine ambao ulipelekea ofisi kufungwa ukimhusisha mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji tukifanya nao kikao na tukatoa maelekezo kwamba kazi ianze na walituahidi baada ya siku Saba watakuwa wameanza kichimba msingi" alisema Msando.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mohammed Fumira amemshukuru Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdulrahaman kwa kuwasaidia kiasi cha shilingi Milion 5.500,000 kwaajili ya ununuzi wa tofali, mchanga pamoja ujenzi wa msingi katika eneo hilo lenye ukubwa wa hekali 10 wakitarajia kujenga pia na nyumba za wahudumu.
Kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Kibaya tunashukuru Sana Mwenyekiti wetu wa achama Cha Mapinduzi kwa kutusaidia kiasi cha fedha shilingi Milion 5.500,000 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati yetu wakina mama walikuwa wanateseka kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya tunaahidi kuikamilisha ujenzi huu kwa nguvu za wananchi"