Na MWANDISHI WETU,
Dodoma. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuhitimisha Bunge Jijini Dodoma, tarehe 28 Juni, 2024.Mazungumzo hayo yalihusu utaratibu wa ulipaji mafao ambao NSSF imeendelea kuuboresha kupitia mifumo ya TEHAMA.
Aidha, Bw. Mshomba ameelezea maandalizi ya ulipaji mafao kwa kuzingatia maboresho ya kanuni ya kikokotoo, na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kujali maslahi ya watanzania.
Pamoja na hayo, Bw. Mshomba alitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti kwa mafanikio makubwa.
Social Plugin