TPC YATOA GAWIO LA BILIONI 69.9 KWA WANAHISA

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro


KIWANDA cha Sukari cha TPC kilichopo mkoani Kilimanjaro ni moja ya viwanda vinavyofanya vizuri kwenye uzalishaji wa sukari baada ya kubinafsishwa na serikali kwenye utawala waserikali ya awamu ya tatu chini ya Rais,marehemu Benjamin William Mkapa.



Tangu kubinafsishwa kwa kiwanda hicho kimeendelea kuipata mafanikio mwaka hadi mwaka nakuendelea kutoa gawio kwa wanahisa wake na kuwa moja ya mlipakodi mkubwa  kwa Taifa.



 Katika  msimu wa kilimo 2022/2023,kiwanda hicho kilizalisha sukari  na kufanya mauzo ya sh,Bilioni 235 na kutoa gawio kwa wanahisa wake lenye thamani ya sh,Bilioni 69.9 huku kikitengeneza faida ya sh,Bilioni 72.7.


Nehemiah Mchechu ni Msajili wa Hazina,anasema  tangu mwaka 2000 kiwanda hicho kimekuwa kikiongeza uzalishaji mwaka hadi mwaka ambapo kwa sasa uzalishaji wa sukari umeongezeka kutoka Tani 36,000 za mwaka 2000 hadi kufikia Tani 116,700 kwa mwaka huu.


Mchechu alikuwa akitoa taarifa ya ufanisi wa uzalishaji wa sukari wa kiwanda hicho kwa wanahisa hivi karibuni mkoani Kilimanjaro na  kueleza ongezeko hilo la uzalishaji wa sukari limetokana na ongezeko la mavuno ya miwa ambapo kwa msimu huo  kiwanda kilivuna miwa zaidi ya Tani 1,150,000.

 
“Katika uzalishaji wa sukari kwa msimu huu, TPC Limited imezalisha zaidi ya tani 116,700 katika kipindi cha juni 2022 hadi machi 2023, hiki ni kiwango kikubwa sana cha sukari  ambacho hakijawahi kuzalishwa katika miaka yote tangu TPC Limited kuanza uzalishaji wake mwaka 1936”.



Anasema wakati wanafanya ubinafsishaji wa kiwanda hicho, serikali ilikuwa imeweka malengo shamba la TPC baada ya kuwa imeongezewa  eneo la shamba la Kahe,  itaweza kuzalisha tani 750,000 kwa mwaka, lakini kwa sasa wanazalisha Tani 1,150,000 ambayo ni juu ya malengo waliyokuwa wamewekwa na serikali wakati wa ubinafsishaji.

 

“Eneo lile lile lakini uzalishaji unazidi kuwa mkubwa kutokana na tija katika uzalishaji kwani kwa mwaka huu  TPC tumeweza kutoa tija ya wastani wa tani 148 (tani mia moja na arobaini na nane)  kwa hekta kiwango ambacho ni cha juu barani Afrika, na ni moja kati ya viwango bora vitatu duniani” anasisitiza Mchechu.


kikiongezeka mwaka hadi mwaka na kuifanya TPC kuongoza kwa miaka mitatu mfululizo kwa kutoa gawio zuri na kubwa serikalini kuliko mashirika mengine yote ambayo serikali ina hisa kidogo”.



Katika hatua nyingine TPC imeanza ramsi mchakato wa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha  uchakataji Molasesi ambacho kitaweza uzalisha bidhaa nyingine ambayo ni spirit kwa ajili ya watumiaji wa viwandani na watumiaji wengine”.
 

Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho(CEO)Marius Jacobs anasema kiwanda hicho kitajengwa TPC na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu na kugharimu sh,Bilioni 100.

 

Anasema  hicho ni kiwango kikubwa cha fedha kitakachowekezwa hatua aliyodai  itakuza zao la miwa na bidhaa zinazotokana na zao la miwa na kwmaba ujenziwakiwnada hicho unataraji kukamilika mwezi Julai mwaka ujao .


Anaeleza kuwa uwekezaji huo kwa TPC utakuza ajira pamoja na kuongeza mapato ya ndani ya kiwanda na kuwezesha kulipa kodi nyingi zaidi na manufaa mengine yatakayopatikana kutokana na uwekezaji huo.


Amesema kiwanda hicho kitazalisha spriti kwaajiliyasoko la ndani pamoja na masoko ya  nje ya nchi.


Kiwanda hicho chaTPC hadi sasa kimeweza kuajiri wafanyakazi 4,000 kiwango inachotajwa kuwa ni  kikubwa sana na ni  makapuni machache ambayo yanawezo kuajiri watu kwa kiwango hiyo.



"Hao ni watu ambao ukiwaangalia mishahara yao imeboreshwa zaidi ya mara mbili ya kima ambacho hulipwa pamoja na bonasi wanachotakiwa wapate,huku wakigharimiwa matibabu pamoja na familia zao”



“Huu ni uwekezaji wa mfano na uwekezaji ambao serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inahitaji,"anasema.



Amesema kama serikali wanajisikia fahari sana kukua kwa uwekezaji wa ndani ya kiwanda hiki cha TPC na kuleta manufaa kwa jamii inayowazunguka kwamba ni azma ya serikali awamu ya sita. 



Anasema kubwa zaidi kutakuwa na ongezeko la uzalishaji wa nishati ya umeme ambapo katika kiwanda hicho wanatarajia kufunga mashine nyingine ya kuzalisha umeme na hivyo kutakuwa na ziada ya megawati Nne hadi saba ambazo zitaingizwa katika gridi ya Taifa.  


 Jafarry Ally ni Mkuu wa Utawala katika kiwanda hicho anasema TPC imeweza kulipa kodi, ushuru pamoja na gawio kwa serikali zaidi ya Sh 99 bilioni, kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kiwango cha Sh 2 bilioni kilichokuwa kikitolewa wakati kampuni hiyo imebinafsishwa mwaka 2000.



Anasema  sababu kubwa ya kuongezeka kwa kiwango hicho ni uzalishaji,mauzo mazuri na ulipaji sahihi wa kodi kwa mujibu wa sheria na miongozo ya ulipaji kodi.



“Mwaka 2010 ndipo kiwanda kilianza kulipa gawio serikali na hadi mwaka 2022/2023 tumekuwa tukilipa gawio na kiwango kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka na kuifanya TPC kuongoza kwa miaka mitatu mfululizo kwa kutoa gawio zuri na kubwa serikalini kuliko mashirika mengine yote ambayo serikali ina hisa kidogo”.,anasema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post