Na Oscar Assenga,TANGA
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) umewataka
wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kujisajili na wakala huo kutokana na
kwamba kama haujasajiliwa hauwezi kuomba tenda rasmi ambazo zinatangazwa na
Taasisi mbalimbali za Serikali na Idara zake.
Hayo yalisemwa leo na Afisa Sheria za Wakala huo Lupakisyo Mwambiga
wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 11 ya Biashara na
Utalii yanayofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini
Tanga.
Lupakisyo alisema kwamba ni vema wafanyabiashara na
wajasiriamali kuona umuhimu wa kurasimisha biashara zao kwa kusajili brela na kupata leseni
inayostahili ili waweze kutekeleza majukumu yao.
“Wengi wanachanganya leseni kati ya daraja A na B ambazo zinatolewa
na halmashauri na Manipsaa kuna biashara zenye sura ya kitaifa na kimataifa unatakiwa
kupata leseni kutoka brela hivyo nawahimiza wafanyabishara waje kupata elimu kwa
kueleza biashara wanazofanya “Alisema
“Kwa lengo la kushauriwa ni leseni gani anapaswa kuomba kutoka
brela na wale wafanyabiashara wenye viwanda vidogo vidogo tunatoa leseni za
viwanda watu wengi hawajua unapoanzisha viwanda lazima uwe na leseni kutoka
Brela”Alisema
Alisema kwamba kuna leseni ya uanzishwaji wa kiwanda na leseni biashara kwa wajasirimali wenye viwanda vidogo
na wafanyabiashara wenye viwanda vikubwa huku akiwataka kutembelea banda lao
ili waone ni vitu gani wanaweza kufanya kupata leseni.
Hata hivyo alisema kwamba wapo kushiriki kwenye maonyesho ya
biashara na utalii kutokana na kwamba ni moja ya taasisi za kusimamia usajili
wa biashara pamoja na leseni na wamekuja kutoa elimu na huduma za papo kwa papo
ikiwemo usajili wa kampuni ,majina ya biashara.
Alisema pia wanatumia maonyesho hayo kutoa leseni kundi A na utoaji wa leseni za viwanda
na usajili wa alama za biashara kwa wateja wao huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kujitokeza
kufika kwenye banda lao ili wawez kupata ushauri jinsi gani wanaweza kusajili
kampuni ,jina la biashara au alama ya bisharaa na waliokuwa tayari wanasajiliwa
kupitia mtandao kwa kuwasaidia kwa sababu wapo kwenye maonyesho na wamekuwa
wakitoa elimu kwa wafanyabiashara umuhimu wa kusajili au kurasimisha biashara maana
wengi mpaka wakipata changamoto Fulani ndio wanakilimbia brela.
“Wengi mpaka wanapopata changamoto ndio wanakimbili brela labda
amepata tenda unatakiwa kupeleka cheti kutoka brela ndio wanahangaika kusajili
au benki wakitaka taarifa kuhusu brela ndio wanakwenda kusajili”Alisema
Social Plugin