RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Wallace Karia amesema kwamba ukarabati unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani utakapokamilika utawezesha uwanja huo kuwa kama wa Benjamini Mkapa wa Jijini Dar es Salaam.
Karia aliyasema hayo leo wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman kuangalia maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo ambao msimu huu utatumika kwa ajili ya michuano ya Kimataifa.
Alisema kwamba shughuli za ukaraibati kwenye uwanja huo tayari umeanza na majani yanayotakiwa kuwekwa hapa ni ya aina ya Babuda na tayari shirikisho la soka nchini watapeleka majani hayo na yapo njiani yanakuja.
Alisema kwa sasa maandalizi kwa ajili ya pichi kwa ajili ya kuondoa majani yaliyokuwepo na udongo yanaendelea na wataalamu wa TFF wataingia leo (Jumamosi) kueleza ni aina gani ya udongo utakaowekwa na jinsi gani ya kuweza kuotosha hayo majani ili yaweze kuota na kuwa na kiwango kinachostahili.
“Majani hayo yatakapokuwa yameota utakuwa ni uwanja huo na wa Benjamini Mkapa ambazo zina majani hayo hivyo kuiwezesha Pichi ya CCM Mkwakwani kuwa kama ya Uwanja wa Mkapa”Alisema Rais Karia
Aidha alisema kwamba suala la vyumba na majukwaa Mwenyekiti nimeshafanya utaratibu wa kumleta mchoraji ambaye amechora na amesema Jumamosi tutapata michoro ya kuweza kurekebisha na tutahakikisha angalau kama Munga atawawezesha uwanja huo tutaweka siti kama wanavyotaka uwanja mzima “Alisema
Hata hivyo alisema kwamba hata kama timu hiyo ikiingia kwenye hatua ya makundi bado timu hizo zitakuja kucheza Tanga Mkwakwani.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhamani alisema kwamba timu ya Coastal Union inatokea mkoani humo na hawana uwanja wenye kukudhi vigezo vya CAF maanake itapelekea timu ya Coastal wanapocheza nchini ikacheze kwenye maeneo mengine nchini nje ya mkoa huo.
“Niwahakikishia wana Tanga kama kiongozi wa kuisimamia Serikali kwenye mkoa wa Tanga na CCM ambayo wanadhamana kubwa ya kumsaidia Rais Dkt Samia Suluhu ambaye anahimiza michezo wa mpira wa miguu na michezo mengine ambaye amejitoa mhanga kuhakikisha mchezo wa mpira wa miguu unakua hapa nchini na kuzisaidia timu mbalimbali lazima tuhakikishe katika mashindano hayo Coastal Union watacheza kwenye mkoa wa Tanga kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani”Alisema Mwenyekiti Rajab
Naye kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union,Hassan Muhsin alisema vita wamepambana kutokushuka daraja zaidi ya mara tatu na sasa wanashukuru Mungu mwaka huu wamepata nafasi ya 4.
“ Lakini tunamhsukuru Mungu msimu uliopita tumepambana kufika nafasi ya 4 na mashindano hayo tulionayo mbeleni yanahitajika maandalizi makubwa sana ule ushirikiano ulikuwepo awali unatakiwa kuzindishwa mara dufu”Alisema
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin