Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CCM TANGA YATAJA VIGEZO VITAKAVYOTUMIKA KUWAPATA WAGOMBEA WA UDIWANI, UBUNGE TANGA 2025



Na Oscar Assenga, PANGANI

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimesema kuwa vigezo ambavyo vitatumika kuwapata wagombea kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka huu na ule Mkuu wa Wabunge na Madiwani wa mwakani 2025 kwamba ni wale ambao wanashiriki kwenye vikao kuanzia ngazi ya mashina.

Vigezo hivyo vilitangazwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman wakati aliposhiriki kwenye mkutano wa Shina namba 5 Mtaa wa Majengo Kata ya Pangani Mashariki ambapo pamoja na mambo mengine alihamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wakati utakapofika.

Katika mkutano huo wa Shina namba 5 Mwenyekiti huyo aligawa viti 100 ikiwa ni kuhakikisha wanakuwa na uchumi imara ambao utawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika shina hilo

Alisema kwamba wanahitaji wapate viongozi ngazi ya serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Ubunge na Madiwani ambao wanakiheshimu chama cha Mapinduzi.

Alisema kwamba tafsiri ya kukiheshimu chama hicho ni kuhudhuria mikutano ya mashina yako na waanapokuwa hawaudhurii maanake bado haujaonyesha kukithamini na kukipenda chama cha mapinduzi.

“Niwaambie kwamba sio hiari ni suala la lazima viongozi wa ngazi za mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa wilaya, Kata na Mitaa na Vitongoji kuhudhuria kwenye mikutano ya mashina na kwa sasa atakayechukua fomu na kujaza na kueleza mikutano ya shina amehudhuria mara tano wakati hajafanya hivyo tutafuatulia maana mikutasari ipo”Alisema

“Sio suala la Hiari ni lazima kuhakikisha viongozi wa ngazi za wilaya wahudhurie mikutano ya shine lake ,Mwenyekiti wa Kata, Mbunge,Diwani hilo ni jambo la msingi linahimizwa kwenye chama chetu lazima wahudhurie kufanya hivyo ndio kukitendea haki chama chetu ujumbe huo ni kwa viongozi wote wa mkoa wa Tanga kwa sababu ndi anadhama nao na wote”Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema kwamba suala la viongozi hao kuhudhuria kwenye mikutano hiyo ya mashina yao sio suala la hiari ni suala la lazima na mtakumbuka wakati najaza fomu kwenye uchaguzi wa chama 2022 ile fomu inavipengelea vingi miongoni mwao ilitaka ueleza vikao ambavyo ulivyoshiriki vya CCM kwa nafasi yako.

“Kwa maana lazima ueleze mikutano ya shina umehudhuria mara ngani kwa maana vikao vya matawi na mikutano mashina umehudhuria mara ngapi hilo ni suala la lazima na mara nyingi tumekuwa tukifanya mazoea kuona jambo la kawaida kawaida”Alisema

“Niwahakikishie uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji na Mkuu wa Mwakani 2025 wa uchaguzi wa kumchagua Rais, Ubunge na Madiwani kipaumbele cha kwanza cha watakaopewa kwenye kugombea ni wale wote ambao wanashiriki vikao na mikutano ya matawi na mashina ya CCM”Alisema

Aidha alisema kwamba atakayejaza fomu na kueleza mikutano ya shina amehudhuria mara tano na hajawahi kufanya hivyo watafuatilia maana mikutasari ipo kwa nafasi hiyo nyeti wanayotaka kumpa huyo mtu wanajua lazima akakiheshimu chama hivyo lazima wapate kumbukumbu zake kwa usahihi na kwa uhakika.

“Kwa hivyo wale wote wanaotarajia kugombea nafasi kwenye chama chao kwenye kura za maoni wajue kama kwenye mashina yao hawakuheshimu vikao vya mashina waliviona havina maana yoyote balozi balozi maana balozi kazi tuliomuachia ni kusuluhusha ndoa za watu”Alisema Mwenyekiti.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com