Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DAWASA YASHIRIKI KONGAMANO LA MAZINGIRA, YASISITIZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI



Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) ni moja ya Taasisi za Serikali zilizoshiriki Kongamano la wadau wa Mazingira kwa lengo la kuongeza uelewa mpana wa usimamizi wa Mazingira linaloratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango wakati akifungua kongamano hilo ameagiza kuangaliwa upya kwa sheria zinazohusu uhifadhi wa mazingira ili kuiwezesha NEMC na Halmashauri kuwa na nguvu ya kuchukua hatua kali dhidi ya uharibifu wa mazingira.

"Kongamano hili limekuja wakati muafaka wa mabadiliko ya tabia ya inchi tumeona mafuriko na ukame katika maeneo mbalimbali duniani ninaagiza Mamlaka husika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa Mazingira pia niwasihi wananchi wenzangu tulinde na kutunza mazingira ili yatutunze" amesema Mhe. Mpango

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Kongamano hilo Mkuu wa Kitengo cha Mazingira Mhandisi Modesta Mushi amesema Mamlaka mbali na usambazaji wa majisafi pia ina jukumu la utunzaji wa vyanzo vya maji ambapo inahusisha utunzaji wa mazingira jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika na DAWASA kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutumiza hilo kwa kubadili fikra kupitia elimu ya mazingira na upandaji wa miti kwenye vyanzo ambapo hadi sasa DAWASA imepanda miti zaidi ya 6000 katika maeneo yote yenye vyanzo vya maji.

" Mamlaka inaendelea na jitihada mbalimbali katika kutunza mazingira ya vyanzo vyetu ambavyo bila hivyo huduma ya usambazaji majisafi haitakuwepo hivyo tunaendelea kusisitiza jamii tutunze mazingira yetu na kwa umuhimu mkubwa tutunze vyanzo ya maji kwa matumizi endelevu na maji ya uhakika" amesema Mhandisi Mushi

Naye,mmoja wa washiriki wa Kongamano hilo Ndugu Lydia Manga mkazi wa Kigamboni amepongeza jitihada zinaendelewa kufanya na DAWASA katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa hasa elimu kwa wafugaji na wakulima wanaoishi pembezoni mwa vyanzo vya maji.

Kongamano hili la Mazingira ni moja ya shamrashamra za kuelekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani Tarehe 5/6/2024 yenye kauli mbiu isemayo "Urejeshwaji wa ardhi Iliyoharibiwa,ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame".


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com