Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga ( aliyekaa katikati)akiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika
Na Mariam Kagenda _Kagera
Serikali Wilayani Muleba Mkoani Kagera imewataka wakulima kulima mazao ya kibiashara ambayo yatawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na kasumba ya kilimo cha mazoea ambacho kimekuwa kikisababisha hali ya utegemezi kwenye jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema hayo wakati akifunga mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika vya matunda na mbogamboga yaliyoandaliwa na tume ya maendeleo ya ushirika (TCDC).
Dkt. Nyamahanga amesema kuwa bado kuna changamoto ya jamii kulima kilimo cha mazoea ambacho hakina tija kwao hivyo kuna haja ya viongozi hao wa ushirika kuhamasisha wakulima kujishughulisha na kilimo cha mazao ya biashara ambacho kitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake mrajisi msaidizi sehemu ya uhamasishaji na uratibu kutoka tume ya maendeleo ya ushirika TCDC Bw. Ibrahimu Kadudu amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaunganisha wakulima wa mboga mboga kuwa ushirika mmoja ambao utawasaidia kupata mbegu na masoko ya uhakika kwa wakati mmoja.
Social Plugin