DKT. YONAZI, TPSF WAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO

 

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Ikiwa ni June 14 ,2024 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na  uongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Raphael Maganga .

Lengo la mazungumzo hayo ni kujitambulisha kwa katibu Mkuu huyo pamoja na kuzungumzia vipaumbele vya Taasisi hiyo, masuala ya kuendeleza sekta binafsi, kutambua fursa za biashara nje ya nchi pamoja na kubainisha vipaumbele vya taasisi na maeneo ya kuimarisha ushirikino na Ofisi ya Waziri Mkuu.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post