MENEJA wa Uhusiano na Mawasiliano Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Titus Kaguo,akitoa elimu kuhusu majukumu ya EWURA wakati wa semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma na kuandaliwa na EWURA Kanda ya Kati.
MENEJA wa Uhusiano na Mawasiliano Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Titus Kaguo,akitoa elimu kuhusu majukumu ya EWURA wakati wa semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma na kuandaliwa na EWURA Kanda ya Kati.
MENEJA wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati Bi.Hawa Lweno,akielezea majukumu ya EWURA Kanda ya Kati,wakati akitoa semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma iliyoandaliwa na EWURA Kanda ya Kati.
BAADHI ya washiriki wakifuatilia semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiliamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma na kuandaliwa na EWURA Kanda ya Kati.
AFISA Huduma kwa Wateja EWURA,Juma Singano,akitoa maelezo kuhusu taratibu za Kusikiliza na Kutatua Migogoro wakati wa semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma iiliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati.
Diwani wa Kati ya Kikuyu Kaskazini Mhe.Israel Mwasansu,akichangia mada wakati wa semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma iiliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati.
MENEJA wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati Bi.Hawa Lweno,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma iliyoandaliwa na EWURA Kanda ya Kati.
MENEJA wa Uhusiano na Mawasiliano Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Titus Kaguo,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma na kuandaliwa na EWURA Kanda ya Kati.
DIWANI wa Kata ya Mbabala Mhe.Pascazia Mayala,akiipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kutoa semina kwa Viongozi,Wadau pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Dodoma kuhusu Mafunzo ya Elimu kwa Umma Juu ya Wajibu na Majukumu ya EWURA iliyofanyika leo Juni 25,2024 jijini Dodoma na kuandaliwa na EWURA Kanda ya Kati.
Na Alex Sonna-DODOMA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati imeonya watu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uuzaji mafuta holela kwenye vidumu huku ukiwataka kuacha mara moja kwakuwa hali hiyo ni hatari kwa maisha yao.
Onyo hilo limetolewa jijini Dodoma na Meneja, EWURA kanda ya kati, Bi.Hawa Lweno , alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya nishati na maji.
Lweno, amesema kuwa tabia ya watu kuuza mafuta holela kwenye vidumu ni hatari kwa maisha yao kwakua maeneo wanayayatumia siyo salama.
“Uuzaji wa mafuta kwenye vidumu na maeneo yasiyo rasmi unaweza kusababisha majanga ambayo yanaghalimu maisha ya watu wengi hivyo nitoe wito kwa watanzania wenzangu kuacha tabia hii ni hatari sana kwetu na kwa wale wanaotuzunguka”amesema Bi.Hawa
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA,Bw. Titus Kaguo, amesema lengo la kikao hicho na wadau hao ni kutoa elimu kuhusu huduma wanazozitoa.
Aidha amesema kuwa , moja kati ya changamoto iliyopo ni ukosefu wa elimu kwa jamii kuhusu huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo.
“Changamoto ambayo imejitokeza Zaidi katika kikao hichi ni pamoja na usomaji wa mita za maji pamoja na upatikanaji wa mkataba wa huduma kwa wateja,”amesema Kaguo
Amesema katika changamoto ya usomaji mita watu wengi hawajui gharama halisi za unit za maji hali ambayo imekuwa ikiibua malalamiko ya kubambikiziwa Ankara za malipo.
“Pia watu bado hawajui umuhimu wa mkataba wa huduma kwa wateja ambao wanaweza kuupata katika mamlaka husika na kuwasaidia kujua haki zao kwa huduma wanazozistahili”amesema Kaguo
Aidha, amesema moja kati ya majukumu ya Mamlaka hiyo ni kulinda mitaji ya wawekezaji na walaji kwa kudhibiti ubora wa bidhaa wanazozizalisha.
“Jukumu mojawapo la EWURA ni kulinda mitaji ya wawekezaji kama mwekezaji atashindwa kupata faida na kufunga uwekezaji basi EWURA itakuwa imeshindwa kutekeleza wajibu wake
Naye Diwani wa Kata ya Mbabala Pascalina Mayala ,ametaka kuwe na sheria ya kuwabana wauza mafuta ambao baadhi yao wamekuwa wakijaza mafuta tofauti na hela wanayolipwa.
Social Plugin