Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAKIELIMU YAZINDUA RIPOTI YA UTAFITI KUHUSU HALI YA UPATIKANAJI WA ELIMU BORA KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAKAZI DUNI NA YASIYO RASMI, MIJINI

Mkurugenzi Uthibiti Ubora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ndg. Ephraim Simbeye, Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu Richard Mabala, Mkurugenzi wa HakiElimu Dkt John Kalage pamoja na wadau wengine wa elimu nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja kuonesha nakala ya ripoti  ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini iliyozinduliwa leo Juni 4, 2024 Jijini Dodoma

NA EMMANUEL MBATILO, DODOMA

SHIRIKA linalojihusisha na Elimu Tanzania, HakiElimu limezindua ripoti ya Utafiti kuhusu hali ya upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini ambayo inakwenda kusaidia kuboresha elimu kwa watoto wenye makazi duni.

Utafiti huo wa HakiElimu umefanywa kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Afrika ‘APHRC’, chenye makao yake makuu jijini Nairobi ambapo utafiti huo umefanyika mwaka 2022 katika mazingira duni ya mijini na umeifikia mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma.

Akizungumza wakati akizindua ripoti hiyo kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, Mkurugenzi Uthibiti Ubora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ndg. Ephraim Simbeye amesema mpango wa Maendeleo ya Sekta Elimu wa Miaka Mitano 2021/22-2025/26 unagusia Elimu ya mjini.

“Mpango huu unatambua kuwa kuna idadi kubwa ya watu wanaohamia mijini kutoka vijijini hali ambayo imesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi mijini ukilinganisha na vijijini. 

Kutokana na hali hii, utafiti huu unatuimiza kuanza kuitumia dhana ya Elimu ya mjini katika mipango yetu”.

“Ni vyema tukatambua kuwa, pamoja na kwamba utafiti huu umelenga makazi yenye kipato cha chini lakini kwa mujibu wa melezo ya Dkt. Kalage dhana ya Elimu mjini ni pana ambayo inagusa mfumo nzima wa upatikanaji wa Elimu mijini”. 

Amesema ni wazi kwamba tofauti zilizopo kati ya mazingira ya mjini na vijiji ndio ambazo zimechangia katika kukuwa kwa dhana hii ya elimu ya mijini.

Vilevile ametoa wito kwa HakiElimu na wadau wengine kuendelea kufanya tafiti na kuziwasilisha kwa umma kwani unatoa nafasi kwa wadau wengi kutumia matokeo hayo katika mipango yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa HakiElimu Dkt John Kalage amesema HakiElimu ilisukumwa kufanya utafiti huo kwa lengo la kupata hali halisi ya upatikanaji wa elimu katika maeneo ya mijini na kuikuza dhana ya elimu ya mjini “Urban Education” kama eneo la kitaaluma na utafiti.

“Katika utafiti huu tulilenga makazi duni au makazi yasiyopangwa. Hata hivyo dhana ya Elimu Mjini ni pana na inagusa utoaji wa elimu mjini kwa ujumla wake. Ni matarajio yetu baada ya uzinduzi huu tafiti nyingi zaidi za kielimu zitafanywa kwenye eneo hili”. Amesema.

Pamoja na hayo amesema changamoto za utoaji elimu mijini ni mtambuka kwani zinahusu maeneo mengi kama vile mipango miji, afya, miundombinu, usafiri, ulinzi na mfumo wa maisha.

Uwasilishwaji wa utafiti huo umefuatiwa na michango kutoka kwa wadau mbalimbali wa Elimu zikiwepo taasisi za serikali na asasi za kiraia, wabunge pamoja na makundi mengi wanaohusika na utetezi kwa elimu hapa nchini.
Mkurugenzi Uthibiti Ubora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ndg. Ephraim Simbeye, Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu Richard Mabala, Mkurugenzi wa HakiElimu Dkt John Kalage pamoja na wadau wengine wa elimu nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja kuonesha nakala ya ripoti  ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini iliyozinduliwa leo Juni 4, 2024 Jijini Dodoma
Mkurugenzi Uthibiti Ubora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ndg. Ephraim Simbeye akizindua Ripoti ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini, Utafiti ambao umefanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo June 4, 2024 Jijini Dodoma

Mkurugenzi Uthibiti Ubora, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ndg. Ephraim Simbeye akizungumza wakati akimuwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda katika  uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini, Utafiti ambao umefanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo June 4, 2024 Jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Bodi HakiElimu, Richard Mabala akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini, Utafiti ambao umefanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo June 4, 2024 Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa HakiElimu Dkt John Kalage akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini, Utafiti ambao umefanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo June 4, 2024 Jijini Dodoma

Mtafiti kutoka APHRC, Francis Kiroro akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini, Utafiti ambao umefanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo June 4, 2024 Jijini Dodoma

Baadhi ya wadau wakishiriki katika hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini, Utafiti ambao umefanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo June 4, 2024 Jijini Dodoma
Baadhi ya wadau wakishiriki katika hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti Kuhusu Hali ya Upatikanaji wa Elimu Bora kwa Watoto Wanaoishi katika Makazi duni na yasiyo rasmi, Mijini, Utafiti ambao umefanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika leo June 4, 2024 Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com