JUMUIYA YA WAZAZI WA CCM YATOA TAMKO KUMHUSU DC WA UBUNGO


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Maganya akizungumza na waandishi wa Habari Leo June 24,2024 Jijini Dodoma. (Picha na Dotto Kwilasa) 

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Maganya amemtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika  kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wazazi kinachotarajiwa  kufanyika Julai  13  mwaka huu  Wilayani Mpanda Mkoani Rukwa.

Amesema Wiki hiyo pamoja na mambo mengine itatumika kupanda miti zaidi ya 100,000 lengo likiwa ni kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kizazi cha sasa na vijavyo. 

Hayo yameelezwa leo Julai 24,2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Maganya wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma na kueleza kuwa ufunguzi wa maadhimisho hayo Julai  8, mwaka huu katika Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mlele kata ya Inyonga kwenye viwanja vya Shule ya msingi Inyonga.

"Tutakuwa na matukio mengi ikiwemo la Julai  10 ambapo tutakuwa na  Baraza kuu la kawaida la Umoja wa Wazazi Tanzania,Julai  11, Julai Kongamano la maadili na Malezi,na Julai 12  itakuwa maalum kwa ajili ya michezo na kauli mbiu ya Sherehe hizo kwa mwaka 2024 ni Uchaguzi 2024/2025, Jumuiya ya Wazazi iko mstari wa mbele, "amefafanua.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo pia ametumia nafasi hiyo kuzungumzia Sakata la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es laam, Hassan Bomboko kutakiwa kuwalipa Mabilion ya Fedha Madada poa 36 waliokamatwa hivi karibuni kwa madai ya kujihusisha na Biashara ya kuuza miili yao.

Amesema wao kama Jumuiya ya Wazazi ya CCM, wanaungana naye kwa kitendo hicho kwani yeye ndiye msimamizi wa Sheria na Maadili katika wilaya anayoiongoza.

Hatua hii imekuja kufuatia hivi karibuni vyombo vya habari kuripoti kuhusu Sakata la ukamataji wanawake 36, wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ukahaba ambapo taarifa ilisema limechukua sura mpya, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC), Hassan Bomboko kupewa notisi ya kuwalipa Sh36 bilioni Mdada poa hao.

Notisi hiyo ya siku 14 inayoanza kuhesabika Alhamisi, Juni 20, 2024, ambayo inalenga kuwalipa watuhumiwa hao 36 wanaodai wamedhalilishwa kwa kuwaita ‘Dada Poa’ na kuwaweka rumande kwa zaidi ya siku tano kinyume na sheria.

Kulingana na hayo Mwenyekiti huyo amesema Jumuiya ya Wazazi ambayo inasimamia maadili kwenye Jamii inamuunga mkoano moja kwa moja Dc wa Ubungo ambaye aliendesha oparesheni ya kuwakamata wanawake hao wanaodhaniwa kuwa madada poa ambao walikutwa katika mazingira ya kuuza miili yao.

“Jumuiya hii tunamuunga mkono DC Hassani kwa Opareshini ile kwani yeye ndiye msimamizi wa sheria katika wilaya yake na alipowakamata hakwenda kama Hassan bali alienda kama kiongozi serikali anapaswa kuhakikisha kunakuwa na maadili katika eneo lake”,amesema na kuongea;


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post