*****************
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
TUZO za makampuni bora barani
Afrika (ACOYA) zilizoandaliwa na The Global CEOs Institute wakishilikiana na
Eastern Star Consulting Group Tanzania zaendelea kuwa chachu ya kuongeza
ufanisi na uzalishaji wa bidhaa bora na zenye viwango ili kuleta tija katika
ukuaji wa maendeleo na uchumi ndani ya Afrika.
Hayo yamesemwa Mei 31, 2024 na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Eastern Star Group of Tanzania Bw. Deogratius John
Kilawe wakati wa hafla ya kuwatunukia Tuzo Makampuni 130 yaliyofanya vizuri
Barani Afrika Kwa mwaka 2024 iliyofanyika katika ukumbi wa The Superdome Masaki
jijini Dar es salaam.
"Lengo ni kutambua mchango
mkubwa wa Makampuni yanayofanya vizuri Barani Afrika na kuwapongeza na kuwapa
moyo ili waendelee kufanya vizuri zaidi ili kuhudumia soko la Afrika Kwa huduma
na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu zitakazoweza kupambana na Soko la Dunia
pamoja na kukuza uchumi wa nchi za Afrika Kwa ujumla' Alisema.
Bw. Kilawe amesema kuwa pamoja
na Mambo mengine ikiwa ni msimu wa 2 wa Tuzo hizo zilizoanza mwaka 2023 na kuleta
mafanikio ya kuwaleta kwa pamoja Makampuni Makubwa zaidi Afrika na Kujadili
mambo mbalimbali yatakayosaidia katika kukuza uchumi wa Afrika pamoja na
kuwatunukia Tuzo Makampuni yaliyofanya vizuri zaidi.
Pia aliongeza kuwa Kwa mwaka
huu ni zaidi ya nchi 20 Makampuni 700 yameshiriki katika Tuzo hizo ambapo zimepatikana Kampuni Bora 130 na
kuwapatia Tuzo ili Kuchochea ufanisi na
katika uzalisha wa bidhaa na huduma.
Tuzo hizo pia zimehudhuriwa na
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Shabani Omary pamoja
na viongozi mbalimbali.
Social Plugin