Na Dotto Kwilasa, Karagwe, Kagera
Kufuatia juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mhe Innocent Bashungwa katika kuimarisha sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Kigasha, Mwandishi wa habari Ndg Mathias Canal amechangia Shilingi Milioni 1 kwa ajili ya madawati.
Mathias amechangia madawati hayo mara baada ya kutembelea shule hiyo iliyopo katika kata ya Rugu, Tarafa ya Nyaishozi akiwa katika kazi ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya kujionea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.
Amesema kuwa usimamizi wa ujenzi wa shule hiyo unaenda sambamba na serikali kupeleka walimu ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Waziri wa Elimu Mhe Prof Adolf Mkenda kwa kuweka kipaumbele katika shule hiyo ili kuhakikisha wanafunzi wa maeneo hayo wanapata elimu bora kama ilivyo katika maeneo mengine.
Kwa upande wake katibu wa Mbunge wa Jimbo la Karagwe Ndg Ivo Ndisanye amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule na upatikanaji wa walimu.
Pia kwa niaba ya Mbunge Mhe Innocent Bashungwa katibu huyo ameahidi kuchangia Mil 3 kwa ajili ya upatikanaji wa madawati ili kuimarisha ufanisi wa kujifunza.
Ivo amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi katika kijiji hicho kwani kupitia nguvu za wanachi wameweza kujenga madarasa mawili ambayo mbunge alitoa mabati kwa ajili ya kupaua.
Social Plugin