Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah kushoto akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Matekelezo Mkoa wa Tanga Wa MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii nchini (NSSF) Abubakari Mshangama |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian kulia akisalimiana na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama wakati alipofika viwanja vya shule ya Sekondari Usagara kufungua Maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batild Burian kulia akipata maelezo kutoka kwa Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama
MKUU wa wilaya ya Muheza Zainab Abdallah akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la NSSF mapema leo wakati wa maonyesho hayo
Na Oscar Assenga,Tanga
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii nchini (NSSF) wameshiriki maonyesho ya 11 hya Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga huku wakiitangaza huduma yao mpya ya NSSF Taarifa.
Akizungumza leo Afisa Matekelezo Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama ambapo alisema mpango huo ni muhimu kwa sababu unamuwezesha mwanachama kupata taarifa binafsi ,michango na madai yake.
Alisema huduma hiyo inapatikana kupitia simu ya kiganjani kwa njia tatu ambazo ni ujumbe mfupi (SMS),Programu ya simu ya Kiganjani (Mobile App) ya NSSF na WhatApp.
“Leo tupo hapa kwenye maonyesho haya pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma zetu lakini pia tunatumia kuitangaza Programu hii inamuwezesha mwanachama kupata taarifa na huduma mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi”Alisema
Aidha alisema pia walikuwa wakieleza mafao yanayotolewa na Mfuko huo na vigezo vyake ikiwemo Mafao ya Pensheni ya Uzeeni ambayo mwanachama hulipwa kila mwezi kwa anayetimiza vigezo vilivyowekwa.
Awali akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la NSSF Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainab Abdallah alisema NSSF ni muhimu sana huku akiendelea kuwashawisha wafanyakazi na wasiowafanyakazi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo ya matibabu na gharura
Alisema wanapoweka akiba yako inakuwa ni rahisi unapokumbana na changamoto mbalimbali inakuwa ni rahisi kuweza kukuhudumia na kukupa matibabu ikiwemo unapofikia umri wa kustaafu unaweza kujilea mwenyewe.
“Niendelee kuwahimiza wafanyakazi na waajiri wajue kwamba ni takwa la kisheria wahakikisha wanawaingiza watumishi kwenye mfuko wa hifadhi za Jamii (NSSF) ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali”Alisema
Social Plugin