RAFIKI SDO YAKUTANA NA MABARAZA YA WATOTO NA WATOA MAAMUZI KUJADILI MPANGO KAZI NA UTEKELEZAJI WAKE NDANI YA HALMASHAURI YA SHINYANGA

Shirika la RAFIKI - SDO limekutana na mabaraza ya watoto na watoa maamuzi kujadili mpango kazi na utekelezaji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Kikao hicho kimefanyika leo Juni 15, 2024 katika ukumbi wa ofisi za Shirika la RAFIKI - SDO zilizopo kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga.

Akieleza lengo la kikao hicho Meneja Mradi wa Kukuza Asasi za Kiraia (MKUA) kutoka Shirika la RAFIKI SDO Maria Maduhu amesema lengo ni kutoa mrejesho wa changamoto na vipaumbele vilivyowasilishwa wa watoto wakati wa kikao  kilichofanyika katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kati ya watoto na watoa maoni.

Amesema miongoni mwa hoja zilizowasilishwa na mabaraza ya watoto katika kikao kilichopita ni pamoja na upatikanaji wa chakula mashuleni, upungufu wa vitabu mashuleni, baadhi ya watoto kukatazwa kwenda shule ili waende kuchunga mifugo, ukosefu wa waalimu, ukosefu wa elimu kwa watoto kwa muda sahihi na kutoshirikisha watoto kwenye vikao vya kufanya maamuzi.

Akitoa mrejesho wa maombi na vipaumbele vya kikao kilichopita upande wa elimu Kaimu Afisa elimu sekondari ambaye pia ni Afisa elimu ya watu wazima Sekondari kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Clement Nyanda amesema upande wa chakula mashuleni kati ya shule 33 ndani ya halmashauri hiyo shule 32 zinatoa chakula kwa wanafunzi mpaka sasa huku Kaimu Afisa elimu msingi ambaye pia ni Afisa elimu ya watu wazima msingi AEWW Christopher Maingu akaeleza hali ilivyo katika shule za awali na msingi ndani ya halmashauri hiyo.

"Katika kuboresha upatikanaji wa elimu na kuhakikisha mtoto anapata chakula awapo shuleni tuliweza kukutana na wazazi na kukubaliana juu ya utoaji wa chakula ambapo mpaka sasa kati ya shule 33 za sekondari shule 32 zimekwisha anza kitoa huduma hiyo, serikali imeendelea kutoa vitabu mwezi wa 5 mwaka huu tulipokea vitabu kwa shule zote 33 zilizopo ndani ya halmashauri yetu", amesema Clement Nyanda.

"Kwa upande wa shule za awali na msingi changamoto inayokwamisha utoaji wa chakula mashuleni ni muitukio mdogo wa wazazi katika uchangiaji ambapo kati ya shule 142 shule 122 pekee ndio zinatoa huduma ya chakula shuleni, tunaendelea kuhamasisha kupitia ngazi za viongozi wa vijiji hadi kata ili wazazi waweze kuvhangia chakula kwa watoto pindi wawapo shuleni, upande wa vitabu vya kufundishia ni kweli tulipokea vitabu lakini changamoto ni utunzaji pamoja na mabadiliko ya mtaala", amesema Christopher Maingu.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Kaimu Afisa mipango halmashauri ya Shinyanga Charles Kato amesema kiasi Cha Shilingi Milioni 16 zimetengwa kwaajili ujenzi na Milioni 180 kw aajili ya ukarabati wa shule kongwe.

"Katika kuboresha miundombinu ya kujifunzia kwa wanafunzi  kiasi cha Shilingi Milioni 180 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe ili kuweka mazingira bora na rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi", amesema Charles Kato.

Meneja Mradi wa Kukuza Asasi za Kiraia (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu akizungumza wakati wa kikao hicho.
Meneja Mradi wa Kukuza Asasi za Kiraia (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki SDO Maria Maduhu akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kaimu Afisa elimu sekondari ambaye pia ni Afisa elimu ya watu wazima Sekondari kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Clement Nyanda akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kaimu Afisa elimu msingi ambaye pia ni Afisa elimu ya watu wazima msingi AEWW Christopher Maingu akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kaimu Afisa mipango halmashauri ya Shinyanga Charles Kato akizungumza wakati wa kikao hicho.
Afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Shinyanga Naomi Paul akizungumza wakati wa kikao hicho.
Picha ya pamoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post