MKUU wa wilaya ya Lushoto Jaffay Kubecha akizungumza mara baada ya kutembelea Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba wilayani humo |
Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba Vyokuta akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya huyo
Na Oscar Assenga, LUSHOTO.KAMPENI ya Rais Dkt Samia Suluhu ya kuhamasisha utalii hapa nchini kupitia Filamu ya Royal Tour imeonyesha mafanikio makubwa kwenye Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba baada ya kupandisha idadi ya watalii kutoka 500 mpaka kufikia watalii zaidi ya 4300.
Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba Vyakuta wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Lushoto Jafari Kubecha akiwa na kamati ya ulinzi na usalama lengo likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani.
Katika ziara hiyo kiongozi huyo wa wilaya alitembelea eneo la kivutio la Maporomoko makubwa ya maji ya Mkuzi Water Falls ambalo limekuwa likitembelewa na wageni wa ndani na nje.
Alisema kwamba kutokana na uwepo wa hamasa hiyo ya Mkuu wa nchi kuhamaisha utalii idadi imekuwa ikipaa sana na mwaka wa fedha 2022/2023 walikuwa na watalii zaidi ya 500 na sasa huu mwezi wa tano wana watalii zaidi ya 4300 .
Alisema hiyo inaonyesha ni jinsi gani utalii unaimarika na tija ya Rais Dkt Samia Suluhu aliyoianzisha inaonyesha jinsi watu walivyoiitikia na wananchi kuitikia kutembelea vivutio vya utalii.
“Lakini pia tunawashukuru viongzi wa wilaya na mikoa na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ambao wamekuwa wakihamasisha watanzania kuja kutembelea huku akiwakaribisha watalii wa ndani na nje kuweza kufika lushoto
Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Lushoto Jaffary Kubecha alisema kwamba katika wilaya hiyo wameanzisha kampeni ya kuhamasisha vivutio vya utalii kutokana na uwepo wa maeneo mengi ya vivutio vya utalii unaosisimua.
Kubecha alisema kwamba watu wengi walikuwa wakisikia Lushoto wanafikiria ni sehemu ambayo ni maarufu kwa Kilimo cha Mbogamboga ikiwemo Kabichi kumbe ni sehemu ya mkakati wa kuvutia watalii.
Alisema kwamba baada ya kutembelea vivutio hivyo ameona namna utalii unavyosisimua kwenye wilaya hiyo lakini bado hawajapata jukwaa rasmi la kutangaza vivutio hivyo kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama na Maafisa utalii wa Halmashauri ya Bumbuli na Lushoto wamejipanga kuanza kutangaza vivutio vya utalii.
Alisema pia kampeni hiyo ya kutangaza vivutio vya utalii inaelekea kwenye shamrashamra za Tamasha kubwa la Lushoto Utalii Festival ambalo litafanyika Julai mwaka huu .
“Lakini hapo katikati kutafuatiwa na Marathon, Water falls tunataka kuiuonyesha dunia na watanzania kwamba Lushoto kuna vivutio vingi hicho ni kimojawapo kwa maana Water falls tulizonazo hapa Lushoto si chini ya tano hii ni mojawapo na misitu ya asili zi chini ya 10”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Aliongeza kuwa pia wana vivutuo vya malikale maeneo ya geographiaya milima,hali ya hewa na majengo ya kale,hotel si chini ya 50 zenye hadhi ya kimataifa dunia na watanzania watambue hilo
“Tupo makini kumuunga mkono Rais Samia Suluhu ambaye wana Lushoto wanamtambuka kama Championi wa Utalii na muda ukifika watampa tuzo ili dunia ijue kwamba lushoto wanatambua kazi nzuri aliyofanya kupitia Royal Tour na namna anavyotembea duniani kutangaza vivutio vya hapa nchini”Alisema DC huyo
Hata hivyo aliwataka watanzania kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii hasa Lushoto kwa sababu wanapokwenda huku wanapata utulivu kwa maana ni sehemu salama ya kumpumzika.
“Lakini bei ni rafiki kwa wazawa badala ya kufikiria msongo wa kutaka kwenda kujinyonga tunaweza kufika Lushoto kwa ajili ya kwenda kupata utulivu wa mwili na akili lushoto ni sehemu salama”Alisema
Social Plugin