SHAKA APIGA MARUFUKU UCHIMBAJI MADINI KWENYE CHANZO CHA MAJI MALOLO

Na Christina Cosmas,  Kilosa

Mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Shaka Hamdu Shaka amepiga marufuku shughuli za uchimbaji holela wa madini, kilimo na ukataji miti hovyo  kwenye chanzo cha maji katika Kata  ya Malolo wilayani humo.

Shaka amesema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi  wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Malolo unaotekelezwa na Ruwasa , ambapo  wananchi hao wamesema  uchimbaji wa madini katika eneo hilo umekua kero na kusababisha uchafuzi wa maji .


Baada ya kupata malalamiko hayo Shaka  amewataka  wananchi kuacha tabia  hiyo na atakaye kamatwa hatua za Kisheria  zitachukuliwa dhidi yake.


Aidha Shaka amewataka wananchi hao kuwa walinzi wa miundombinu hiyo Ili iwanufaisha Kwa kipindi  kirefu  kizazi Cha Sasa na kijacho kwani serikali inatumia gharama kubwa kuwafikishia huduma  hiyo wananchi

Anasema serikali imekua ikitekeleza ujenzi wa miradi Mbalimbali kwenye sekta ya maji  hivyo baadhi ya watu  wamekua na  wakiharibu miundombinu hiyo.


"dokta samia Suluhu Hasaan amekua akitoa fedha kwenye miradi ya maji hasa wilaya hii ya Kilosa hivyo lazima tutunze miundombinu hii na Kila mtu awe mlinzi wa mwezake", amesema


Awali mmoja wa wakazi wa Malolo Boazi Igombe ameishukuru Serikali Kwa ujenzi wa mradi huo  kwani awali walikua wakipata  huduma hiyo umbali mrefu  Lakini Bado Changamoto ya shughuli za  uchimbaji madini katika chanzo cha maji  zinarudisha nyumba  jitihada za serikali huku wakihofia Kupata magonjwa ya mlipuko.


Kwa Upande wake Meneja Wakala wa maji safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Kilosa Mhandisi Silvia Ndimbo amesema ujenzi wa mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi Bil.1 na utawanufaisha Wakazi zaidi elfu 13 wa vijiji vya Malolo A,Malolo B  na Chabi.


Mradi wa maji Malolo umejengwa kwa Fedha za COVID 19  na ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2022/2023 chini ya mkandarasi Jeccs Contruction and Supplies limited  na sasa mradi imekamilika kwa asilia 100  tayari umeanza kutoa huduma kwa Wananchi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post