MKURUGENZI wa huduma saidizi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mathias Mhembe,akizungumza kwenye Banda la TBA katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
MTUMISHI kutoka Shirika Umeme Tanzania (TANESCO),Salama Kasamaru,akiupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kupata elimu katika banda la TBA katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Na.Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa huduma saidizi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mathias Mhembe, amesema wataendelea kushirikiana na sekta binafsi kufikia malengo yaliyowekwa na serikali
Bw.Mhembe, ameyasema hayo kwenye Banda la TBA katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Amesema kuwa katika kutekeleza maagizo ya serikali Wakala huo utaendelea kushirikiana na sekta binafsi kukamilisha malengo mbalimbali yaliyowekwa na serikali.
"Wakala wa Majengo Tanzania unayo majukumu matatu ya kuteleza ikiwemo kujenga nyumba za serikali,kutoa ushauri wa ujenzi wa miradi ya majengo mbalimbali yanayojengwa lakini pia kusimami miliki za serikali"amesema Bw.Mhembe
Aidha, ameeleza lengo la kushiriki maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ni kutoa huduma za moja kwa moja kwa wananchi ili wapate mrejesho kwa ajili ya kufanyia kazi.
"Tupo hapa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali lakini pia kupata mrejesho wa huduma zetu ambazo tunatoa kwa wanachi ili tuweze kufanyia kazi yale mapungufu ambayo tutaelezwa"amesema
Hata hivyo amesema TBA, wanaendelea kutumia mifumo mbalimbali ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) iloyo andaliwa na serikali kutoa huduma kwa wateja.
"Lakini pia tunatumia mifumo hiyo kwa ajili ya watumishi wetu ukiwemo ule wa kupima utendaji kazi wa watumishi wetu ili kutoa huduma bora kama mkataba wa huduma kwa wateja unavyotutaka"amesema
Bw.Mhembe amesema kuwa mkataba wa huduma kwa wateja unawataka kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje.
"Hivyo basi nitowe wito kwa watanzani na wageni kutoa nje kuja kupata huduma bora zinazozingatia takwa la mkataba wa huduma kwa wateja"amesema
Naye Mtumishi kutoka Shirika Umeme Tanzania (TANESCO),Salama Kasamaru,ametoa rai kwa watumishi wa umma kuitumia TBA kujenga nyumba ili kuondokana na usumbufu wa mafundi mtaani.
" Mimi nilikuja hapa kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu miradi ya ujenzi wa nyumba kwa watumishi Bunju, lakini bahati mbaya nyumba zile zimeisha lakini mradi mwingine utakapoanza nitahakikisha napata nyumba na nitoe rai kwa watumishi wenzangu kuitumia TBA ili kukwepa usumbufu wa mafundi mtaani"amesema