Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughuikia Idadi ya Watu (UNFPA), wameendesha zoezi la utafiti shirikishi wa kijamii (PAR) katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu kuiwezesha jamii kuibua, kuchambua na kuweka mikakati ya kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika jamii.
Uraghibishi huu unafanyika katika kata za Murusi na Kumsenga zilizopo Halmashairi ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma. Zoezi hili limehusisha wananchi kutoka katika vikundi vya wanawake na wanaume zaidi ya 30, na washiriki wapatao 50.
Uraghibishi huu unatumia mbinu shirikishi ya Uibuaji, Uchambuzi na kuweka mipango ya Utekelezaji (U-3) katika kubaini sababu za tatizo la Ukatili wa kijinsia na kuweka mikakakti ya kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.
Hii ni sehemu ya Utekelezaji wa Mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa, chini ya UNFPA, wilayani Kasulu, unaolenga pia kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto ili kuwawezesha kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.
Social Plugin