Na Oscar Assenga,TANGA
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanazingatia sheria za utoaji wa risiti halali wakati wa utoaji wa huduma bila kushurutishwa.
Hayo yalibainishwa leo na Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Mkoa Tanga,Flavian Byabato kwenye maonyesho ya 11 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Usagara jijini Tanga.
Alisema kwamba lazima wafanyabiashara watambua kwamba ni muhimu sana kuhakikisha wanatoa risiti wakati wa utoaji wa huduma kupitia jina la kampuni halisi kupitia mashine za kieletroniki.
Aidha aliwataka wafanyabiashara wapya kuhakikisha wanajisajili na kama hawajui namna ya kujisajili wafike kupatiwa elimu kwa kuwa maonyesho hayo ya kitaifa kuna wageni wengi ambao wanatoka mikoani na nje ya nchi na wafike ikiwemo kupewa elimu ya namna bora ya kutumia mashine na ulipaji kodi kwa hiali na ushauru wa Forodha.
Hata hivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti ikiwemo kwa wanunuzi kudai risiti halali na kiasi halisi alicholipia kupitia jina la biashara hata kama ni ya kuandikiwa kwa mkono.
Social Plugin