UHAKIKI WA NHIF YABAINI WANACHAMA ZAIDI YA 13O SIO HALALI KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA TANGA

Na Oscar Assenga, TANGA


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga katika zoezi la uhakiki wa wanachama kwenye vituo vya kutolea huduma umebaini uwepo wa wanachama zaidi ya 130 ambao sio halali

Hayo yalibainishwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Evans Nyangasa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini humo

Alisema uhakiki huo ulifanyika kati ya mwezi June 2023 mpaka sasa na katika udanganyifu huo kuna baadhi ya waliotumia huduma hizo wameweza kuzilipia gharama ambazo walitumia ndivyo sivyo huku wakitoa wito kwa watoa huduma kutoa kwa mwanachama sahihi na kwa wakati sahihi na huduma halali.

“Tumejipanga kutoa huduma kwa wananchi kwenye nyumba za ibada,mashule na vijiji ili waweze kujiunga na bima ya afya lengo lao ni kuhakikisha kila mwananchi anajiunga na mfuko huu"Alisema 

Alisema lengo lao ni kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu juu ya matumizi mazuri ya kadi ya bima ya afya kutokana na kwamba siku za karibuni kumeibuka miongoni mwa wanachama wanashiriki udanganyifu kutumia kadi zao ndio sivyo jambo ambalo linapelekea mfuko kutumia gharama nyingi.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhakikisha wanatumia kazi zao vizuri wanapokwenda kwenye vituo vya kutolea huduma ndio maana Tanga tumejipanga kuendelea kuweka watalaamu kwenye vituo vya kutolea huduma kwa lengo la kudhibiti udanganyifu ambao unaweza kutokea wakati wa utoaji wa huduma na nisisitize wananchi waendelea kuzingatia miongoozo na taratibu za huduma”Alisema

Hata hivyo alisema wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa watanzania juu ya huduma zinazotolewa ikiwemo umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa wananchi kutokana na kwamba inawapa uhakika wa kugharamia gharamaza za matibabu bila kulipia gharama za ziada.

“Pamoja na kutoa elimu lakini pia tunapokea malalamiko na maoni kutoka kwa wanachama wetu juu ya huduma zinazotolewa na mfuko na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu na kuwa na huduma bora kwa wanachama wa pale wanaponufaika na huduma hizo”Alisema

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa akizungumza Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania Saady Kambona na Meneja wa Tarura Mkoa wa Tanga kulia wakati walipotembelea banda lao katika viwanja vya Usagara Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya Biashara na Utalii 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa akizungumza Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania Saady Kambona na Meneja wa Tarura Mkoa wa Tanga kulia wakati walipotembelea banda lao katika viwanja vya Usagara Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya Biashara na Utalii 
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga Shymaa Kwegyir kulia akipatiwa huduma kwenye Banda la NHIF 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian kulia akisalimiana na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Evans Nyangasa wakati alipokwenda kufungua maonyesho ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Usagara Jijini Tanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post