Na Mwandishi wetu _ Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amezindua Mashindano ya mpira wa wavu Kanda ya Ziwa Magharibi yanayohusisha timu kutoka mikoa minne.
Mashindano hayo yamefanyika leo Juni 29, 2024 katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo DC Mtatiro ametoa wito kwa wadau wa michezo kuendelea kuunga mkono mchezo wa mpira wa wavu kama ilivyo kwenye michezo mingine.
"Kwanza niwakaribishe katika wilaya ya Shinyanga, ujio huu unatupatia chachu ya kufanya maboresho kwenye viwanja vyetu vya michezo, kwa niaba ya serikali niwatakie kheri ya mashindano haya na yajayo kwa timu ambazo zitafanikiwa kufuzu kwenda kushiriki mashindano ya kitaifa, lakini pia niendelee kutoa wito kwa wadau wa michezo kuweka nguvu kwenye mpira huu wa wavu kwani mpira huu ni mzuri na umetoa fursa za ajira kwa vijana wengi", amesema DC Mtatiro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mpira wa Wavu Kanda ya Ziwa Magharibi Jason Rwekaza amesema lengo la mashindano hayo ni kutafuta timu mbili zitakazo kwenda kushiriki kwenye michuano ya kitaifa itakayohusisha timu 14 wanaume na 10 wanawake kutoka kutoka kanda zote hapa nchini.
"Michuano hii ni kwa ajili kutafuta washindi wawili wa kwenda kushiriki mashindano ya Tanzania Volleyball National League - TVNL inayotarajia kuanza tarehe 22/07/2024 huko jijini Dar es salaam", amesema Jason Rwekaza.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa wavu Tanzania Laurence Safari amesema mashindano hayo ya kanda ya mpira wa wavu yatatoa nafasi kwa washindi kwenda kushiriki mashindano ya kitaifa lakini pia mshindi wa kitaifa atafuzu kwenda kushiriki mashindano ya ligi ya mabingwa ya mpira wa wavu na kuongeza kuwa dhamira ya mashindano hayo ni kuinua mpira wa wavu hapa nchini.
Mwenyekiti wa Mpira wa wavu kanda ya ziwa magharibi Jason Rwekaza akizungumza wakati wa mashindano hayo.
Katibu mkuu wa chama cha mpira wa wavu Tanzania Laurence Safari akizungumza wakati wa mashindano hayo.
Mashindano yakiendelea.
Mashindano yakiendelea.
Mashindano yakiendelea.
Baadhi ya watazamaji waliojitokeza kwenye mashindano hayo.
Mashindano yakiendelea.
Mashindano yakiendelea.
Social Plugin