Muonekano wa maboma mawili yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi wa vitongoji vya Kyabunyonyi na Samo Kata ya Kisumwa Wilayani Rorya Mkoani Mara
Muonekano wa Shule ya Msingi Kyabunyonyi
Na; Frankius Cleophace _ Rorya
Miongoni mwa vitu ambavyo vinasaidia watoto kupenda shule na pia kumuwezesha mtoto kujifunza na kuelewa kwa haraka ni mazingira yaliyo rafiki kwa mtoto kuanzia miundo mbinu ya shule na hasa madarasa.
Miundombinu isiyo rafiki kwa mtoto si tu inachangia mtoto kutokupenda shule na kuongeza tatizo la utoto bali pia imekuwa inaathiri ukuaji uwezo wa mtoto kujisomea na kuelewa kwa wakati.
Wilayani Rorya Mkoani Mara katika Shule ya Msingi Kyabunyonyi iliyopo kata ya Kisumwa inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa jambo ambalo lisasababisha wanafunzi wa madarasa mawawili tofati kutumia chumba kimoja wakati wa ujifunzaji hali ambayo inahatarisha maendeleo ya awali ya mtoto kiakili.
Kwa mujibu wa sayansi ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto umri kati ya miakia 0-8,Suala la ufundishaji watoto wa umri huu linaitaji wanafunzi kuwa na madarasa ya kutosha yenye mahitaji yote yatakayomsaidia mtoto kuelewa kwa haraka na kusaidia ukuaji wa ubongo .
Wambura Masare kwa niaba ya Mwalimu mkuu shule ya msingi Kyabunyonyo alisema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 522 Wavulana274 na wasichana 248 vyumba vya madarasa 05 na jumla ys walimu wakiwa 6 huku Mwalimu wa kike akiwa mmoja kati ya walimu hao shuleni hapo hali inayohatarisha ustawi wa ukuaji wa mtoto mwenye umri chini ya miaka nane kiakili.
Licha ya wanafunzi wa awali kutumia darasa moja bado darasa la pili na la tatu wanalazimika kusoma kwa zamu ambapo darasa moja linakuja asubuhi na linginie mchana jambo ambalo limekuwa linaathiri muda sahihi wa mtoto chini ya miaka nane kukaa darasani na kupata huduma nyingine za shuleni ikiwemo michezo.
Alisema kuwa wanafunzi watano wa shule ya awali na wale wa msingi wanalazimika kutumia dawati moja na wakati wa kufanya mitihani hali ambayo inamnyima mtoto nafasi ya utulivu.
Kwa kuona changamoto hiyo wananchi wa vitongoji viwili Samo na Kyabunyoni Kata ya Kisumwa wilayani Rorya wanalazimika kujenga vyumba viwili kwa nguvu zao ili kutatua changamoto hiyo ambavyo vimefikia usawa wa lenta nakuomba sasa wadau na serikali kuwaunga Mkonno ili kukamilisha ujenzi huo ii pale wanafunzi watakapofungua shule wakute madarasa hayo yamekamilika kwa lengo la kutatua changamoto hiyo.
Katika kuunga mkono Nguvu za Wananchi hao Mkurugenzi wa Kiwanda cha Nyihifa Sunflower na mlezi wa shule hiyo anaopongeza nguvu za wananchi wa vitongji hivyo viwili Samo na Kyabunyoni kujitoa kwa ajili ya ujenzi huo.
“Nawapongeza sana kwanza wananchi kwa kutumia nguvu kazi zenu kujenga mpaka mdarasa yanafikia hatua hii kubwa mimi kama mzawa wa vitongoji hivi na mlezi wa shule nitakamilisha ujenzi wa madarasa haya ili kupunguza changamoto inayokabili shule hii” alisema Nyihita.
Vile vile Nyihita alisisitiza sasa jamii kuendelea kupeleka shule bila kuwa na ubaguz nakulaani pia vitebdo vya ukatili ambavyo vinatokea hapa Nchini.
Zablon Segere ni diwani kata ya Kisumwa alichangia kiasi cha shilingi Milioni moja pamoja na madawati Kumi kuunga mkono jitiada za wananchi hao kwa ujenzi wa vyumba hivyo.
Chacha Simon ni mkazi wa kitongoji cha Samo kata Kisumwa alisema kuwa sasa serikali ione umhumu wa kukamilisha vyumba hivyo licha ya wadau kujitokeza kusaidia wananchi.
“Vile vile Miundombinu ya barabara ni mibovu hatuna madarada mvua zikinyesha wanafunzi hawa wadogo tunalazimika kuwafuata shuleni ili kuwavusha sasa ni chagamoto tunaomba pia serikali itusaidie” alisema Chacha.
Shule hiyo kwa sasa ina madawati 100 huku hitaji likiwa ni madawati 240 ili kufanya mazingira ya kuseomea kwa watoto wente umri chini ya miaka 8 kuwa shawishi na rafiki kama mpango jumuishi wa taofa wa malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto unavyoelekeza.