WALIOSOMA SHYCOM WARUDISHA SHUKRANI NYUMBANI

Mratibu wa kamati ya maandalizi ya mbio za marathon za Shycom Alumni Arnold Bweichum akiwa na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CIG )  Charles Kichele .  

 Na Dotto Kwilasa,Malunde Blog 1 Dodoma

UMOJA wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Ualimu Shinyanga(SHYCOM)wametoa rai kwa Wanafunzi wengine waliomaliza Chuoni hapo kuungana kwa pamoja kuchangia na kusaidia shule hiyo kupitia Mbio za Shycom Alumni Marathon zitakazo jumuisha kilometa 5, 10 na 21 ambazo zitaenda kufanyika kwa mara ya kwanza Septemba 21 mwaka huu Mkoani hapo.

Mratibu wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Arnold Bweichum amezungumza hayo leo June 20,2024 jijini Dodoma kwenye mkutano wake na vyombo vya habari ambapo ameeleza  lengo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule ya Sekondari Shycom iliyopo Mkoani 
Shinyanga. 

Aidha amesema pamoja na mambo mengi yaliyoandaliwa,mbio hizo pia zitahusisha kuibua vipaji vya watoto ambao watakuja kuwa na mchango mkubwa kwenye mchezo wa riadha nchini ikiwa ni pamoja na kuinua kiwango cha Elimu nchini. 
Amesema, "Tunaimani mbio hizo zinakwenda kuibua vipaji kwani makundi malimbali yatashiriki mbio hizo bila kusahau wanafunzi wanaosoma chuoni hapo na waliomaliza chuoni hapo, " Amesema Bweichum. . 

Bweichum ameongeza kuwa, " Shycom imetoa mazao mengi, wengi wao ni viongozi wakubwa katika Serikali ya Tanzania hivyo katika mbio hizo tunakwenda kurudisha shukrani katika shule yetu kwa kusaidia pale panapo stahili lakini pia michezo ni afya, ajira hivyo tunategemea mazuri kupitia mbio hizi, " Amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Riadha Mkoa wa Shinyanga Reuben Shampamila amesema lengo ya mbio hizo ni kufanya hamasa, umoja na mshikamano kwa wanafunzi wa Shycom
Kwani ni ukweli kwamba Shycom ilikuwa kumbilio la kuwajenga vijana kuwa viongozi bora. 
" Tumeona tusiiachie Serikali peke, tutashikamana kuinua elimu nchini, kupitia mbio hizi tunakwenda kuboresha miundombinu ili wanafunzi waliopo na watakokuja kuweza kusoma sehemu yenye mazingira salama ,"amesisitiza

Ametaja Ada za mbio hizo kuwa ni pamoja na mshiriki anatakiwa kulipa shilingi 35000 ambapo shilingi 30000 vitaghalamia vifaa vya marathon na shilingi 5000 itaenda shuleni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati unaohitajika. 

Naye  Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CIG )  Charles Kichele akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliomaliza chuo cha Ulimu Shinyanga amesema wanatakiwa kurudisha shukrani katika shule yao kwani bila SHYCOM  pengine wasinge kuwa viongozi wakubwa. 

" Turudishe shukrani kwa ajili ya vizazi vya sasa na vya baadae kupitia  mbio hizi tunakwenda kufanya jambo kubwa na lakihistoria, " Amesema







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post