Na Mwandishi Wetu, Kagera
Watuhumiwa tisa wa mauaji ya mtoto Asimwe Novart aliyekuwa na ualbino ambaye aliibwa nyumbani kwao Kamachumu may 30 mwaka huu 2024 ambapo June 17 mwaka huu 2024 mwili wake ulikutwa kwenye kalavati akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vyake,leo wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba wakiwa chini ya ulinzi mkali kwa ajili ya kusomewa mashtaka yao
Mkuu wa mashtaka Mkoa wa Kagera Waziri Mangumbo akisaidiana na wakili wa serikali Erick Mabagala wamewasomea mashtaka yao watuhumiwa hao tisa kuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya makusudi huku akisema kuwa uchunguzi wa shauri hilo no 17740 la mwaka 2024 tayari umekamilika
Shitaka hilo limesomwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba Elipokea Yona Wilson ambaye amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote na wamerudishwa rumande mpaka July 12,2024 ambapo kesi yao itatajwa tena
Watuhumiwa hao tisa ni Elpidius Alfred Rwegoshora miaka 49 ambaye ni padri,Novat Venant miaka 24 ambaye ni baba wa mtoto,Nurdin Ahmada,Ramadhan Selestine,Rwenyagira Alphonce,Dastan Buchard, Faswiu Athuman,Gozibert Arikad na Dezdery Everigist