WENYE ULEMAVU, WANAWAKE, VIJANA WAHAMASISHWA KUJIANDIKISHA KUWA WAPIGA KURA


Mjumbe wa Tume, Jaji (Rufaa) Mhe. Mwanaisha Kwariko akizungumza wakati akifungua mkutano wa Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu, uliofanyika leo tarehe 11 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Alifungua Mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Seleman Mtibora akiwasilisha mada kwenye mkutano wa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, na kusema uboreshaji wa daftrai pamoja na mambo mengine utahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.








Na. Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa wito kwa makundi mbalimbali katika jamii wakiwepo watu wenye Ulemavu, wanawake na vijana kutumia majukwaa, taasisi na mashirika yao kuhamasishana kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.


Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume, Jaji (Rufaa) Mhe. Mwanaisha Kwariko kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu, uliofanyika leo tarehe 11 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.


Mkutano huo umefanyika sambamba na mkutano wa Tume na wawakilishi wa wanawake na wawakilishi wa watu vijana ikiwa ni mwendelezo wa mfululizo wa vikao kama hivyo vilivyofanyika kuanzia tarehe 07 Juni, 2024.


Jaji Mwanaisha Kwariko alisema Wawakilishi wa watu wenye ulemavu mnayofursa ya kuwahamasisha wenzao kwenye majukwaa yao.


"Hivyo, nawasihi na kuwaomba kwa dhati mtumie fursa hizo wakati wote mnapotangaziana mambo mbalimabli, moja ya matangazo yawe kuwahamasisha watu wenye ulemavu kujitokeza kujiandikisha kuwa wapiga kura," amesema Jaji Kwariko.


Jaji Kwariko amewashukuru wawakilishi wa watu wenye ulemavu kwa ushirikiano mkubwa ambao wameuonesha kwa Tume wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.


“Kwenye mazoezi ya uboreshaji wa Daftari yaliyopita, watu wenye ulemavu mmekuwa msaada mkubwa katika kuhamasisha na kuelimisha wananchi haswa kundi lenu la watu wenye ulemavu kupitia majukwaa mbalimbali," amesema.


Pia, amewashukuru watu wenye ulemavu kwa kujitokeza kwa wingi kiasi ambacho kimeiwezesha Tume kufikia malengo yake ya kuandikisha wapiga kura na kuwaomba waendelee na utamaduni huo.


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Seleman Mtibora akiwasilisha mada kwenye mkutano wa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima R. K amesema uboreshaji wa daftrai pamoja na mambo mengine utahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.


Ameongeza kuwa zoezi hilo pia litatoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka Kata au jimbo walioandikishwa awali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post