THPS YASHIRIKI KATIKA KAMPENI YA ‘AFYA YANGU, HAKI YANGU’ MAARUFU AFYA CODE CLINIC SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kushoto) akiipongeza THPS kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuimarisha afya za wananchi pamoja na kuwapatia elimu ya kujikinga na maradhi mbalimbali alipotembelea Banda la THPS wakati wa maadhimisho ya kampeni ya "Afya Yangu, Haki Yangu" iliyopewa jina la Afya Code Clinic Mkoani Shinyanga yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga Julai 25,2024. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kushoto) akizungumza alipotembelea Banda la THPS 
Meneja Programu wa THPS Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Amos Scott  akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kushoto) kuhusu huduma za afya zinazotolewa na THPS
Mshauri wa Ubora wa Huduma za Afya Mradi wa Afya Hatua THPS Makao Makuu, Agnes Kirato (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kuhusu huduma za afya zinazotolewa na THPS


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Siku ya Afya Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 7 Aprili. Mwaka huu, wadau wanaadhimisha siku hiyo kwa kuendesha kampeni ya "Afya yangu, Haki yangu"  ili kupigania haki ya kila mtu kupata huduma bora za afya.

Mkoani Shinyanga shughuli za kuadhimisha siku hiyo zinafanyika katika viwanja vya Kambarage kuanzia tarehe 24 hadi 27 Julai 2024 kupitia Kampeni iliyopewa jina la Afya Code Clinic iliyoandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  kwa kushirikiana na wadau wa afya.

Kupitia mradi wa Afya Hatua unaofadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC), Tanzania Health Promotion Support (THPS) inashiriki katika maadhimisho hayo kwa kutoa elimu na huduma za afya kwa wakazi wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo yanayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Meneja Programu wa THPS Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Amos Scott amesema maadhimisho hayo yanayoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma za afya, watekelezaji wa miradi na vyuo vya afya yanalenga kuhamasisha tabia ya kutafuta huduma za afya na kutoa huduma bora za afya kwa wakazi wa Shinyanga.

Dkt. Scott amesema katika maadhimisho hayo,THPS inatoa huduma za kupima VVU, afua za kinga, uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Meneja Programu wa THPS Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Amos Scott.

Dkt. Scott amesema THPS katika Mkoa wa Shinyanga inahudumia zaidi ya Wapokea huduma za VVU 71,183 katika vituo 92 vya Tiba na Matunzo ambapo asilimia 99% kati yao wameweza kufubaza Virusi vya UKIMWI lakini pia THPS kwa Kushirikiana na Serikali katika kipindi cha Oktoba 2023 - Juni 2024 imetoa huduma ya upimaji wa VVU kwa watu 211,763 na kati yao zaidi ya 4077 walikutwa na maambukizi ya VVU na wote wamewaunganisha katika huduma za tiba na matunzo.

Ameeleza kuwa katika kipindi cha Oktoba 2023 hadi Juni 2024, wapokea huduma 21,759 walipimwa saratani ya mlango wa kizazi, ambapo 563 waligundulika kuwa na viashiria vya saratani hiyo na 552 kati yao walipatiwa matibabu.

“Tunaendelea kuwaokoa akina mama dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi. Tunaomba wanawake wajenge tabia ya kupima afya zao kwani saratani nyingi zikiweza kufanyiwa uchunguzi wa awali zinatibika, isipotibiwa mapema ni ngumu kutibiwa”,amesema Dkt. Scott.

Kadhalika, amesema THPS hutoa huduma za afya mahususi kwa vijana. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2024, mradi wa Afya Hatua umetoa huduma kwa vijana 4,027 wanaoishi na VVU ambapo 3,082 ni wanawake na 1,125 ni wanaume. THPS inafanya kazi na vituo mbali mbali vya kutolea huduma za afya ili kuhakikisha matumizi sahihi ya dawa za kufubaza VVU kwa wapokea huduma.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, akiwa katika banda la THPS, amewapongeza wadau hao kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuimarisha afya za wananchi pamoja na kuwapatia elimu ya kujikinga na maradhi mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

"Kwanza niwapongeze kwa kazi kubwa mnayofanya na sisi tunawashukuru , ni vizuri kuwa na maeneo kama haya kwa maana ya kwamba tunataka watu wakimbilie kwenye maeneo yanayotoa elimu kwa sababu elimu ndiyo tiba ya kwanza halafu kupima ni tiba ya pili halafu inayofuata kushauriwa ya tatu ni matibabu. Kama watu wangetumia muda mwingi kupata elimu mambo mengi tungeweza kuyaepuka",amesema Mhe. Macha.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga amewakumbusha wananchi kuwa ugonjwa wa UKIMWI bado upo na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya ngono ikiwemo Homa ya Ini yapo hivyo vijana wawe makini wachukue hatua za kujikinga lakini pindi wanapobainika kuwa na maambukizi ya VVU wazingatie matumizi ya dawa za kufubaza makali ya VVU.

"Nimeona THPS mnafanya huduma ya Tohara Kinga kwa wanaume. Ndugu zangu Tohara Kinga siyo jambo la siri wananchi jitokezeni kupata tohara Kinga",amesema Mhe. Macha.


Kuhusu THPS

Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 2011, chini ya Sheria ya asasi zisizo za kiserikali nambari 24 ya 2002.

THPS inafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara za Afya za Tanzania Bara na Zanzibar; Wizara ya Jinsia, Vijana, Wazee na Makundi Maalum; Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Misaada ya UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (U.S. CDC), THPS inatekeleza afua mbalimbali za VVU/UKIMWI; Kifua Kikuu; kuzuia ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto; huduma za afya ya uzazi, uzazi, watoto wachanga, watoto na vijana; mifumo ya habari ya maabara na usimamizi wa afya, na UVIKO-19.

Kuhusu mradi wa CDC/PEPFAR Afya Hatua (Oktoba, 2021- Septemba, 2026)

Mradi huu unalenga kutoa huduma jumuishi katika vituo vya afya (Kigoma, Pwani, Shinyanga na Tanga) na katika jamii (Kigoma, Pwani na Tanga).

Huduma hizi ni pamoja na matibabu na matunzo ya watu wanaoishi na VVU, huduma za kitabibu za tohara kwa wanaume katika mikoa ya Kigoma na Shinyanga na programu ya DREAMS kwa wanawake katika mkoa wa Shinyanga.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mshauri wa Ubora wa Huduma za Afya Mradi wa Afya Hatua THPS Makao Makuu, Agnes Kirato (kulia) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kuhusu huduma za afya zinazotolewa na THPS
Mshauri wa Ubora wa Huduma za Afya Mradi wa Afya Hatua THPS Makao Makuu, Agnes Kirato (kulia) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kuhusu huduma za afya zinazotolewa na THPS
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiwa katika banda la THPS linalotoa huduma rafiki kwa vijana ikiwemo upimaji wa VVU, uchunguzi wa magonjwa ya ngono, utoaji wa dawa Kinga (PrEP), uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza na uchunguzi wa kifua kikuu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiwa katika banda la THPS linalotoa huduma rafiki kwa vijana ikiwemo upimaji wa VVU, uchunguzi wa magonjwa ya ngono, utoaji wa dawa Kinga (PrEP), uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza na uchunguzi wa kifua kikuu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiwa katika banda la THPS linalotoa huduma rafiki kwa vijana ikiwemo upimaji wa VVU, uchunguzi wa magonjwa ya ngono, utoaji wa dawa Kinga (PrEP), uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza na uchunguzi wa kifua kikuu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiwa katika banda la THPS linalotoa huduma rafiki kwa vijana ikiwemo upimaji wa VVU, uchunguzi wa magonjwa ya ngono, utoaji wa dawa Kinga (PrEP), uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza na uchunguzi wa kifua kikuu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiwa katika banda ya THPS linalotoa huduma za upimaji wa VVU
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiwa katika banda ya THPS linalotoa huduma za upimaji wa VVU
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiwa katika banda ya THPS linalotoa huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama
Wananchi wakiendelea kupata huduma kwenye banda ya THPS linalotoa huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama
Huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama zikiendelea katika Banda la THPS
Huduma za afya zikiendelea kutolewa katika Banda la THPS

soma pia 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post