Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akipima uzito na urefu wakati akifungua rasmi Kampeni ya Afya Code Clinic inayofanyika katika viwanja vya CCM Kambarage Mjini Shinyanga inayoendeshwa na Jambo Fm Radio kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili kuchukua hatua za mapema pindi wanapobainika kuwa maradhi.
Mhe. Macha ametoa rai hiyo leo Julai 25,2024 wakati akifungua rasmi Kampeni ya Afya Code Clinic ya utoaji matibabu bure ambayo imeratibiwa na Kampuni ya Jambo Group Limited kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa udhamini wa benki ya CRDB.
Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya huduma za Afya zinazotolewa kupitia kampeni hiyo ili kupata huduma za matibabu na kuimarisha afya zao.
Aidha ameishukuru kampuni ya Jambo Group na Jambo Fm Radio kwa kuamua kushirikiana na ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa kutoa huduma za Afya bure kwa wananchi na kuelezea dhamira ya serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya.
Mhe. Macha amewakumbusha wananchi kuwa ugonjwa wa UKIMWI bado upo na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya ngono ikiwemo Homa ya Ini yapo hivyo vijana wawe makini wachukue hatua za kujikinga lakini pindi wanapobainika kuwa na maambukizi ya VVU wazingatie matumizi ya dawa za kufubaza makali ya VVU.
Aidha amepongeza juhudi zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suhuhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za matibabu ya Kibingwa hadi katika ngazi za halmashauri nchini hatua aliyoelezea kuwa imerahisisha ufikishaji wa huduma hizo kwa karibu zaidi kwa wananchi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt .Yudas Ndungile amesema kupitia kampeni hiyo ya Afya Code Clinic wananchi wanapata huduma za matibabu bure, elimu za afya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.
Naye Meneja Mkuu wa Jambo Media ambaye pia ni Kiongozi wa Chapa na Matangazo wa Jambo Group Bw. Nickson George amesema lengo la utekelezaji wa kampeni ya Afya Code Clinic ni kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za matibabu bure huku akieleza kuwa walizalisha wazo la kuanzisha Kampeni kupitia vipindi vyao vya kijamii katika eneo la afya ili kuimarisha afya ya jamii.
Kupitia Kampeni ya Afya Code Clinic iliyoanza Julai 24,2024 ikitarajiwa kufikia tamati Julai 27,2024 jumla ya vipimo vya magonjwa 15 yakiwemo yanayohitaji huduma za kibingwa vinaendelea kufanyika katika viwanja vya CCM Kambarage katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua rasmi Kampeni ya Afya Code Clinic inayofanyika katika viwanja vya CCM Kambarage Mjini Shinyanga inayoendeshwa na Jambo Fm Radio kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati Kampeni ya Afya Code Clinic inayofanyika katika viwanja vya CCM Kambarage Mjini Shinyanga inayoendeshwa na Jambo Fm Radio kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Meneja Mkuu wa Jambo Media ambaye pia ni Kiongozi wa Chapa na Matangazo wa Jambo Group Bw. Nickson George akizungumza wakati Kampeni ya Afya Code Clinic inayofanyika katika viwanja vya CCM Kambarage Mjini Shinyanga inayoendeshwa na Jambo Fm Radio kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

soma pia
AFYA
THPS YASHIRIKI KATIKA KAMPENI YA ‘AFYA YANGU, HAKI YANGU’ MAARUFU AFYA CODE CLINIC SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kushoto) akiipongeza THPS kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuimarisha afya za wan…
AFYA
BENKI YA CRDB YASHIRIKI AFYA CODE CLINIC - MATIBABU BURE KWA WANANCHI SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kushoto mwenye shati jeupe) akiwa katika Banda la Benki ya CRDD leo Julai 25,202…
AFYA
RC MACHA ATEMBELEA BANDA LA CHUO CHA AFYA KOLANDOTO - MAONESHO YA AFYA CODE CLINIC
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kulia mwenye shati jeupe) akiwa katika Banda la Chuo cha Sayansi Kolandoto kilic…
HABARI
RC MACHA AIPONGEZA JAMBO GROUP, JAMBO FM KUFANIKISHA KAMPENI YA AFYA CODE CLINIC 'MATIBABU BURE KWA WANANCHI'
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akipima uzito na urefu wakati akifungua rasmi Kampeni ya Afya Code Clinic inayof…
Social Plugin