RC MACHA AFUNGA MAONESHO YA AFYA CODE CLINIC KWA MDAHALO WA MASUALA YA AFYA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye mdahalo huo.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamingi Macha, amefunga rasmi maonesho ya afya code clinic kwa mdahalo wa kujadili mada mbalimbali ya kiafya, huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuelekeza nguvu zaidi kwenye utoaji elimu kwa wananchi kujikinga dhidi ya magonjwa kuliko kutanguliza tiba.

Macha akizungumza wakati wa kuhitimisha maonesho hayo, amesema kampuni ya jambo imefanya jambo jema kwa kuandaa maonyesho hayo,sababu imekuwa ni utalii wa matibabu na pia wananchi kupata elimu ya kiafya.
"Mdahalo huu nimeupenda sana ni tiba kubwa ya kuzuia magonjwa, wananchi ukiwapatia elimu utapunguza idadi kubwa ya wagonjwa, na hapa wananchi wamepata elimu dhidi ya kujikinga na magonjwa na kinga ni bora kuliko tiba," amesema Macha.

Ametoa wito pia kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwamba wajenge pia utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara pamoja na kupata matibabu mapema.
Aidha, ameelezea pia mafanikio katika sekta ya afya kipindi cha utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan mkoani humo, kwamba ametoa fedha Sh.bilioni 34.7 na kuboresha huduma za afya ikiwamo ujenzi wa hospitali,vituo vya afya,zahanati na ununuzi wa vifaa tiba.

Amesema kwamba imejengwa hospitali ya Rufaa mkoani humo,hospitali tatu mpya,vituo vya afya 20, Zahanati 50,ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa, huku watumishi wa afya na madaktari 640 wakiajiriwa pamoja na ujenzi wa nyumba Sita za watumishi wa afya.
Meneja Mkuu Jambo Media Nickson George,ameishukuru Serikali mkoani humo kwa kushirikiana nao kikamilifu kufanikisha maonesho hayo na kutoa huduma za matibabu kwa wananchi.

Amesema kwamba lilikuja wazo la kuanzisha Afya Code Clinic ndipo wakaona watutafute wadau wa kushirikiana nao,na kukutana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa mkoa huo wanakuwa na maisha mazuri na wenye afya njema.
"Kuwa na maisha mazuri siyo tu pesa nguzo ya maisha mazuri ni afya, na sisi kama Kampuni ya Jambo tutaendelea kuanda matukio kama haya kila mwaka, na tunatarajia pia kufanya iwe ya Afrika Mashariki ili kuimarisha afya za wananchi,"amesema Nickson.

"Tutatafuta kila mbinu na kufanya ubunifu wa kila namna, ili kuufanya mkoa wa Shinyanga unakuwa sehemu ya utalii na "event"hii wananchi wamefanya utalii wa kitabibu licha ya kufanyiwa uchunguzi wa afya zao na kupata matibabu,"ameongeza.
Aidha,amesema ndani ya siku hizo nne za afya code clinic,wananchi zaidi ya elfu 7 wametembelea na kupata huduma za kiafya.

Pia, amewapongeza Madaktari,watoa huduma wote wa afya na wadau mbalimbali wa maendeleo,kwa kujitoa kwao na kuwapatia huduma za matibabu wananchi elimu ya afya ili kujikinga na magonjwa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga dk.Yudas Ndungile,amesema baada ya kuletewa wazo hilo na kampuni ya jambo la afya code clinic, wakajadiliana na kisha kuandaa utoaji huo wa huduma za matibabu,na kutafuta pia madaktari bingwa wakiwamo kutoka hospitali ya Aga khan.

Amesema licha ya utoaji wa huduma za hizo za matibabu,wakaja na wazo pia la kufanya mdahalo ili wananchi wajadili kwa pamoja mafanikio ya sekta afya na changamoto zake.
Katika mdahalo huo zimejadiliwa mada mbalimbali ikiwamo ya ustawi wa jamii na lishe, magonjwa yasiyo ya kuambukizi na afya ya akili, magonjwa ya vvu,mlipuko na yasiyo ya kuambukiza.

Mada zingine ni afya ya uzazi,elimu ya afya kwa umma na mafanikio ya sekta ya afya kipindi cha Rais Samia Suluhu Hassan iliyo ongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Maonesho hayo ya afya code clinic yalianza kutolewa kuanzia Julai 24 na yamehitimisha leo Julai 27 yakiratibiwa na kampuni ya jambo group limited,kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na ufadhili pia wa benki ya CRDB.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye mdahalo huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.Yudas Ndungile akizungumza kwenye mdahalo huo.
Meneja Mkuu wa Jambo Media Nickson George akizungumza kwenye mdahalo huo.
Meneja Mkuu wa Jambo Media Nickson George akizungumza kwenye mdahalo huo.
Uwasilishaji wa mada ukiendelea kwenye mdahalo huo.
Uwasilishaji wa mada ukiendelea kwenye mdahalo huo.
Uwasilishaji wa mada ukiendelea kwenye mdahalo huo.
Uwasilishaji wa mada ukiendelea kwenye mdahalo huo.
Washiriki wakiwa kwenye mdahalo huo.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Vyeti vya pongezi kwa wadau vikitolewa kufanikisha maonesho ya afya code clinic.
Vyeti vya pongezi kwa wadau vikitolewa kufanikisha maonesho ya afya code clinic.
Vyeti vya pongezi kwa wadau vikitolewa kufanikisha maonesho ya afya code clinic.
Vyeti vya pongezi kwa wadau vikitolewa kufanikisha maonesho ya afya code clinic.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha (kushoto) akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kufunga maonesho ya afya code clinic.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha (kushoto) akiendelea kusalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kufunga maonesho ya afya code clinic.
Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha (kushoto) akiendelea kusalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kufunga maonesho ya afya code clinic.
Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha (kushoto) akiendelea kusalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kufunga maonesho ya afya code clinic.
Picha za pamoja zikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post