HII NDIYO BAISKELI YA KWANZA KUTENGENEZWA DUNIANI

Baiskeli ya kwanza kutengenezwa duniani
Baiskeli ya kwanza duniani ilitengenezwa na Karl Drais raia wa Ujerumani mwaka wa 1817, askari wa msituni ambaye alikuwa na elimu ya Fizikia na Hesabu.

Mwaka huo, Drais aliiendesha kwa mara ya kwanza mashine hiyo aliyoipa jina 'Laufsmaschine'. Kulingana na wasifu ulioandikwa na Dkt. Gerd Hüttmann.

"Mnamo Juni 12, 1817 Karl Friedrich Christian Ludwig, Freiherr (= baron) Drais aliiendesha baiskeli aliyoivumbua ya magurudumu mawili, maili tano kutoka katikakati mwa Mannheim na kurejea katika muda chini ya saa moja. Ilikuwa baiskeli bila ya vikanyagio lakini mtu alihitaji kutumia miguu yake kuisaidia kwenda, ilikuwa yenye kasi kuliko kutembea. Aliiita Laufmaschine (mashine iliyokimbia Ujerumani) lakini vyombo vya habari viliiita 'Draisine' kutokana na jina lake."

Kilichomsukuma kuvumbua baiskeli hiyo kimeelezwa kuwa kukabiliana na mgogro wa kimazingira uliokuwa umetokea wakati huo. Alitaka madala wa kutumia farasi ambao walikuwa wakitumiwa siku hizo.
Farasi wengi walichinjwa kwa sababu palikosekana chakula cha kuwalisha na wakaliwa na wafugaji wao kwa kuwa nao pia walikuwa hanawa chakula.

Baron Karl von Drais alitaka kukitumia kifaa chake bila ya kuwahusisha farasi na wanyama wengine ambao walikuwa wameangamizwa na njaa iliyokuwa imetokea. Drais aligundua kuwa, kwa kuweka magurudumu katika fremu za mbao alizokuwa ametengeneza, angefanikiwa kuipanda na kuidhibiti. Lloyd Alter aliandika kupitia jarida la Tree Hugger.

Kuweza kufika katika shamba lake na kufanya shughuli zake bila ya kuchoka, kuliifanya Laufsmaschine kuwa baiskeli ya kwanza dunia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post