Na Sumai Salum - Kishapu
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, kimempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Joseph Mkude na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Emmanuel Johnson kwa usimamizi mzuri wa utekelezwaji ilani ya Chama hicho kwa zaidi ya asilimia tisini na tano (95%) katika miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo.
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 10,2024 na viongozi na wajumbe wa Halmashauri kuu ya wilaya kupitia kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za CCM Kishapu baada ya uwasilishwaji wa hoja za utekelezaji ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari-Juni 2024 na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Joseph Mkude.
Akisoma taarifa ya utekelezaji ilani Mkuu wa Wilaya huyu Mhe. Mkude amesema ushirikishwaji katika kipindi chote cha utekelezaji kuanzia ngazi ya wananchi,tawi na kata wamekuwa tayari kukagua na kusiamamia miradi hivyo kupelekea kuimarika kwa utekelezaji miradi mbalimbali inayotekelezwa kuwa bora siku hadi siku.
Aidha miradi hiyo iliyokamilika kwa zaidi ya 95% ni pamoja na Elimu Sekondari,Elimu msingi,Afya,Maji,Barabara,Umeme,Kilimo umwagiliaji pamoja na ushirika, Maendeleo ya jamii,Biashara viwanda na uwekezaji,Mipango na uratibu,Utawala na utumishi, Fedha,Mawasiliano serikalini,Tehama,Uhifadhi taka ngumu na usafi wa mazingira,Maliasili na uhifadhi wa mazingira,Misitu(TFS) pamoja na Idara ya Ardhi.
"Nipende kutoa pongezi kwa Mbunge wetu Butondo asiyelala bungeni kwa ajili ya wanaKishapu, Mkurugenzi wangu na watumishi wote walio chini yake, Madiwani,Taasisi zisizokuwa za serikali ikiwemo World Vision na Redeso,wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa ushirikiano wao wanaonipa katika kuwatumikia wananchi" ,ameongeza Dc Mkude.
Aidha Mhe. Mkude ametoa pongezi kwa Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo kuwa kielelezo cha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutoa majiko zaidi ya 145 kwa wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya hiyo.
"Pongezi kwa Mbunge wetu kwa kutambua na kutekeleza ajenda ya serikali ta awamu ya sita ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na ameahidi kuendelea kutuletea majiko ya gesi ili idadi ya watumiaji nishati safi ya kupikia iwe kubwa kwani ziko athari nyingi za Nishati chafu kama mkaa na kuni ikiwa ni pamoja na athari kiafya kwa watumiaji,uharibifu wa mazingira na pia ni gharama", amesema Mkude.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo amempongeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kwa umoja wa kufanya kazi na kutekeleza ilani huku akiongeza kuwa amesema kuwa yuko bega kwa bega na serikali pamoja na Chama kuhakikisha maendeleo kwa wananchi wa Kishapu yanapatikana kwani tangu alipoingia madarakani mwaka 2020 hadi sasa 2024 miradi kwenye maeneo mbalimbali imetekelezwa huku akisema serikali kupitia mfuko wa jimbo itaendelea na inaendelea kufanya mambo makubwa Kishapu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. Emmanuel Johnson amesema kuwa kutokana na fedha za serikali kuu na mapato ya ndani watahakikisha wanasimamia vema kutekeleza miradi ya maendeleo na kuibua miradi mipya yenye tija kwa wananchi hivyo kila mwakilishi wa wananachi ahakikishe anasimamia vizuri upatikanaji wa mapato na kuhakikisha hayapotei kwani hayuko tayari kumvumilia mtu yeyote atakae kwamisha zoezi la ukusanyaji mapato hasa wanapoelekea kuzindua kituo cha afya cha Mwamalasa na miradi mingine maeneo tofauti tofauti.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo Leo julai 10,2024 katika ukumbi wa ofsi za Chama hicho walipokuwa kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya cha uwasilishwaji hoja za utekelezaji ilani Januari- Juni 2024 akizungumzia mikakati ya ofisi ya Mbunge kwa serikali kuu ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Kishapu na namna ilivyotekelezwa kuanzia mwaka 2020 kuelekea 2025 na namna amejitoa kuipigania jamii yote ya Kishapu bila kujali tofauti za imani na vyama vyako.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Mkude akizungumzia madhara yayokanayo na matumizi ya nishati chafu ya mkaa,kuni na kinyesi cha mifugo kwa matumizi ya kupikia majumbani huku akielezea mipango ya Mbunge wa jimbo hilo na serikali ya awamu ya sita katika kutekeleza suala la matumizi ya nishati safi ya kupikia kabla ya zoezi la ugawaji leo Julai 10,2024 katika ofIsi za CCM Wilayani humo baada ya kuwasilisha hoja za utekelezaji ilani ya Chama hicho januari-juni 2024 iliyotekelezwa kwa zaidi ya 95% mpaka sasa.
Mbunge jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo (kushoto), Mjumbe wa Halmashauri kuu Bi.Francisca Bahame (katikati),na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Mkude akikabidhi majiko ya gesi kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo leo Julai 10,2024 katika viwanja vya ofsi za CCM Wilayani humo.
Zaidi ya majiko 145 yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Bonipace Butondo kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilayani humo kwa lengo la kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia leo Julai 10,2024 katika viwanja vya ofisi ya Chama hicho Wilaya.
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao hicho
Katibu wa Siasa na Uenezi Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Bw. Jiyenze Seleli akizungumza kwenye kikao cha uwasilishwaji hoja za utekelezaji ilani ya Ccm Wilaya
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga , Shija Ntelezu akizungumza kwenye kikao hicho
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, Francis Mashenji akizungumza kwenye kikao hicho
Mjumbe baraza kuu la Wanawake CCM Taifa Bi.Christina Siwango akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga chenye lengo la kupokea hoja za utekelezaji ilani ya CCM Wilaya iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Joseph Mkude
Social Plugin