Mkamba Herbs(JRM)📿
Tabia Hatarishi zinazomfanya mtu anakuwa katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo
- Kutokupata chakula kwa wakati.
- Matumizi ya pombe na sigara.
- Kuwa na msongo wa mawazo, stress na hofu.
- Matumizi ya marakwamara yadawa zunazopelekea uzalishwaji mkubwa wakiwango cha acid tumboni(HCl), mfano Aspirin.
MADHARA YA VIDONDA VYATUMBO.
👉Uvujaji wa damu ndani ya utumbo: Hali hii yaweza kusababishwa na vidonda kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya damu kuanza kuvuja. Hali hii ni hatari sana na inahitaji tiba ya dharura.
👉 Vidonda vya tumbo huweza kusababisha tundu (kutoboka kwa ukuta wa tumbo) na kufanya vitu vilivyo ndani ya utumbo kutapakaa katika tumbo (abdomen) Hali hii huitwa peritonitis na ni hatari sana na inahitaji matibabu ya dharura. Aidha, kuenea huko kunaweza pia kuathiri tezi kongosho na kusababisha madhara katika tezi hiyo, ugonjwa unaojulikana kama pancreatitis.
👉Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani kama vile ini au kongosho (pancrease)
👉Kuvimba kwa kuta za tumbo pamoja na makovu yanayosababishwa na vidonda hivi huweza kusababisha kuziba kwa njia ya kupitishia chakula kutoka kwenye tumbo (stomach) kwenda sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenum) hali ambayo kitaalamu huitwa gastric outlet obstruction.
👉 Iwapo vidonda vya tumbo vimesababishwa na H. pylori, kuna uwezekano wa kati ya mara tatu hadi ya sita ya mgonjwa kupata kansa ya tumbo (stomach cancer).
ILI TUEPUKANE NA VIDONDA VYA TUMBO LAZIMA TUFANYE YAFUATAYO:
👉Tuwe na tabia ya kula chakula kwa wakati.
👉 Tuepuke matumizi ya muda mrefu ya madawa ya kuzuia inflamesheni(inflammation) kama vile Aspirin.
👉Tule mlo kamili.
👉 Tuwe na tabia ya kufanya mazoezi.
👉 Tuache matumizi ya pombe na sigara.
👉 Tufanye uchunguzi mara kwa mara na kupata matibabu kwa wakati.
👉 Tuepuke hali ama vitu vinavyotufanya tupate msongo wamawazo na stress.
- MKAMBA HERBS(JRM)
- VISOMO DUWA NA DAWA
- DAWA ZA KIARABU ASILI KIGOMA
+255755705090📿
Social Plugin