KATAMBI AKUTANA NA WAZEE MANISPAA YA SHINYANGA, "TUNA IMANI NA WEWE, USITETEREKE NA MANENO YA WAKOSAJI"

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu akizungumza alipokutana na Wazee kupitia Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga na Baraza la Wazee CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga limeeleza kuwa na imani na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kutokana na utendaji wake kazi wa kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo na kutatua matatizo ya wazee.

Wamebainisha hayo leo Julai 13,2024 wakati Mbunge Katambi alipofanya Mkutano na Wazee wa Manispaa ya Shinyanga, kuchota busara zao ili aendelee kuwa kiongozi bora.

Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano, akisoma andiko la wazee wamempongeza Mbunge Katambi namna wanavyochapa kazi ya kuwatumia wananchi na kuwaletea maendeleo na kwamba ndani ya miaka minne ya Ubunge wake, Shinyanga imekuwa na maendeleo makubwa.

"Tunakupongeza Mbunge wetu Katambi kwa kazi kubwa ambayo unaifanya hapa Shinyanga,pamoja na Serikali kwa ujumla chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan, kwa kutujali pia wazee na hata kuunda mabaraza ya ushauri ya wazee kuanzia ngazi za chini kabisa na kushughulikia matatizo yetu", amesema Tano.

Aidha,wazee hao kupitia andiko lao wameiomba Serikali kusaidia kuinua ustawi wa maisha ya wazee,ulinzi, kupata huduma bora za matibabu yakiwamo madawa ya wazee na vitambulisho vya matibabu bure.

"Wazee tunakabiliwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,na magonjwa haya yanatuua sana,tunaomba Serikali iboreshe huduma na kutupatia matibabu bure, sababu wazee hawana fedha za kulipia gharama za matibabu,"amesema Tano.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Benard Itendele,amemtaka Mbunge Katambi kwamba aendelee kuchapa kazi na asitetereke kutokana na maneno ya wakosaji na kwamba mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe.

"Ukiwa kiongozi ni jalala,maneno ya wakosaji hayakosekani hasa kwa kiongozi mchapakazi kama wewe, nawaomba wazee tumuunge mkono kijana wetu Katambi,"amesema Itendele.

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha, amewaambia wazee hao kwamba wana Mbunge mchapa kazi na mwenye nidhamu, sababu anathamini watu wa rika lote na leo amekutana na wazee.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe, amewaomba wazee hao kwamba wasisite pia kufika kwenye Ofisi za CCM kutoa ushauri,na kwamba watawatumia pia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa , ili kupata wagombea wazuri na wenye sifa.

Katambi akizungumza kwenye kikao hicho, amesema amekutana na wazee hao ili kuchota busara zao, sababu wazee ndiyo dira ya nchi na kwamba kiongozi yoyote atakayedharau wazee hawezi kuwa kiongozi bora na taifa litaangamia.

"Wazee ndiyo waliolifikisha taifa letu hapa,na leo nchi ina amani na utulivu na sisi tumekuwa viongozi sababu ya nyie wazee na hata Rais wetu Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anawapenda sana, na changamoto zenu zote zitaendelea kutatuliwa,"amesema Katambi.
Mhe. Patrobas Katambi.

Amewaomba pia wazee kulipigia kelele na kulikemea tatizo la Mmomonyoko wa maadili,ambalo limekuwa tatizo duniani kote ambalo linakwenda kupoteza taifa na hata kuja kukosa viongozi bora.

Ametumia pia fursa hiyo kuwaomba wazazi,kuacha malezi ya kisasa kwa watoto,ambayo ndiyo yamekuwa moja ya tatizo la mmomonyoko wa maadili kwa vijana.

Amewatoa hofu wazee hao kwamba Serikali chini ya Rais Samia wataendelea kuboresha huduma za matibabu na kwamba katika Manispaa ya Shinyanga zimetolewa fedha nyingi ikiwamo ujenzi wa hospitali na ununuzi wa vifaa tiba na madawa ya magonjwa ya wazee.

Katambi pia amewaeleza wazee hao miradi ya maendeleo ambayo ameitekeleza kwa kipindi chake cha Ubunge ndani ya miaka minne kwamba ahadi zake alizoziahidi nyingi ametekeleza.

Katika Mkutano huo wazee pia walipewa kila mmoja jiko la gesi kwa ajili ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha, kwenye Mkutano huo wazee walikuwa wakiimba nyimbo za kuwa na imani na Mbunge Katambi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu akizungumza na Wazee kupitia Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga na Baraza la Wazee CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumamosi Julai 13,2024 katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu akizungumza na Wazee kupitia Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga na Baraza la Wazee CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini

Mwenyekiti wa  Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga na Baraza la Wazee CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Tano Stephano (kulia) akikabidhi Andiko la Wazee kuhusu ajenda mmomonyoko wa maadili kwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu 

Mwenyekiti wa  Baraza la Ushauri la Wazee Manispaa ya Shinyanga na Baraza la Wazee CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Tano Stephano akizungumza kwenye mkutano huo

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Benard Itendele akizungumza kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) na wazee Manispaa ya Shinyanga 

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anold Makombe akizungumza kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) na wazee Manispaa ya Shinyanga 

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Hamisa Hassan Chacha akizungumza kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) na wazee Manispaa ya Shinyanga

Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye Mkutano 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post