Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikiendelea kukagua Gati la maji Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga mjini ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Mhe. Anord Makombe imeridhishwa na miradi mitano (5) iliyotekelezwa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Hayo yamebainishwa leo Jumatano Julai 24,2024 baada ya kamati hiyo kutembelea na kukagua miradi hiyo mitano yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni moja.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Mhe. Anord Makombe ameipongeza SHUWASA kwa kuimarisha huduma ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa wakati na kushughulikia changamoto za wateja huku akiwahimiza kuendeleza ushirikiano huo.
“Mimi niwapongeze SHUWASA mnajitahidi sana lakini lipo eneo ambalo tumeona mmefanya vizuri japo halijafika kwa asilimia mia moja pamoja na ubora wa huduma za SHUWASA, mamlaka ya majisafi SHUWASA tumeona mtandao karibia kila eneo umefika lakini kwenye changamoto za kukatika kwa maji mnajitahidi kutoa taarifa mimi niwaombe tu muendelee kuongeza wateja kwa sababu tunapoongeza wateja na kipato kinaongezeka ili mamlaka iweze kustawi zaidi ya hapo tuendelee kuwa na ushirikiano tufanye kazi wote kama timu”,amesema Makombe.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko naye ameipongeza SHUWASA kwa kuyafikia maeneo yote ya Manispaa ya Shinyanga huku akiwasisitiza kuendelea kuzingatia suala la usafi katika maeneo ya miradi pamoja na kushughulikia kwa haraka changamoto pale zinapojitokeza kwa wananchi.
“Nawapongeza sana kwa sababu maeneo yote ya Manispaa yamefikiwa na maji kwahiyo vimebaki tu vile viunganishi kutoka hapa kwenda pale lakini kazi mnafanya vizuri na mnahitaji pongezi kubwa sana niendelee kuwatia moyo watumishi wa SHUWASA kazi wanazozifanya ni kubwa maana zinaonekana”,amesema Mhe. Masumbuko.
Wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini pamoja na mambo mengine wameridhishwa na miradi hiyo mitano ambayo wameitembelea huku wakiisisitiza mamlaka hiyo kuendeleza ushirikiano uliopo kwao na wateja wao.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya maji ambayo ilikuwa ni kero kwao huku wakiipongeza SHUWASA kwa kuendelea kuwashirikisha katika hatua mbalimbali kwa lengo la kuimarisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya ameitaja miradi ambayo imetembelewa na kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa mtandao wa bomba na vituo vya kuchotea maji kijiji cha Bugwandege ambapo amesema mradi huo tayari umekamilika na kwamba wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.
Amesema mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba kijiji cha Bugimbagu umekamilika kwa asilimia mia moja ambapo tayari wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama, ujenzi wa mtandao wa bomba na kituo cha kuchotea maji kijiji cha Magwata mradi umekamilika pamoja na upanuzi wa mdandao wa bomba Ngelegani, Ndala na Butengwa tayari wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.
Pia amesema mradi wa ujenzi wa mdandao wa bomba na kituo cha kuchotea maji kijiji cha Mwanubi umekamilika na wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama huku akiendelea kuwakumbusha wananchi kutunza miundombinu ya miradi hiyo ili iweze kuduma. Viongozi na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakipata maelezo ya miradi kabla ya kuanza ukaguzi.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya akifungua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na vituo vya maji kijiji cha Bugwandege Manispaa ya Shinyanga.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na vituo vya maji kijiji cha Bugwandege Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akielezea chemba ya Valve ya mtandao wa maji.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikikagua Gati la maji Bugwandege leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikikagua Gati la maji Bugwandege leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akiandika ushauri unaotolewa na mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya na Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa wakiandika ushauri unaotolewa na mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akielezea chemba ya Valve ya mtandao wa maji.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya akielezea mradi huo katika kijiji cha Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiwa amefungua maji.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikiendelea kukagua Gati la maji Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na vituo vya maji kijiji cha Magwata Nhelegani Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Mhe. Anord Makombe akiwasili katika Gati la maji kijiji cha Magwata manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akipata ufafanuzi katika Gati la maji Magwata Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba kijiji cha Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akitoa maelezo ya mradi katika Gati la maji Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Nsianeli Gerald akiwa katika Gati la maji Bugimbagu kata ya Mwawaza.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikiendelea na ukaguzi wa miradi.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya akizungumza.
Kikao cha majumuisho kikiendelea baada ya kutembelea na kukagua miradi mitano.
Social Plugin