Hyderabad, India - Mwanafiziotherapia mwenye umri wa miaka 32, aliyekuwa ameajiriwa katika hospitali moja huko Hyderabad amekamatwa kwa madai ya kumuua mkewe na binti zake wawili wachanga.
Uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa mshukiwa huyo alihusika katika uhusiano wa nje ya ndoa na muuguzi kutoka hospitali moja.
Akiwa amechochewa na nia yake ya kuendelea na uhusiano huo, inadaiwa aliamua kuiondoa familia yake.
Kulingana na mamlaka, mwanamume huyo alimchukua mkewe na binti zake hadi Raghunadhapalem mandal katika wilaya hiyo, ambapo kwanza alitoa dozi yenye sumu ya kufisha ganzi kwa mke wake wa miaka 26.
Baadaye, alidaiwa kuwanyonga binti zake wa miaka minne na wa miaka miwili na nusu, kama NDTV ilivyoripoti.
Mwanamume huyo wa Hyderabad alifanya nini baada ya kudaiwa kuua familia?
Katika kujaribu kufanya vifo hivyo vionekane vilitokana na ajali, mshukiwa aliuweka mwili wa mkewe kwenye kiti cha nyuma cha gari lao, na kuwaweka watoto wake kwenye viti vya mbele na kuligongesha gari hilo kwenye mti makusudi.
Hata hivyo, uchunguzi wa kisayansi ulibaini kutoendana na hali inayodhaniwa ya ajali.
Aidha polisi walieleza kuwa mshtakiwa alijaribu kuficha ushahidi wa kitaalamu unaomhusisha na mauaji hayo baada ya kutekeleza kitendo hicho.
Social Plugin