Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AWESO AZIAGIZA MORUWASA NA BONDE KUSHIRIKIANA KUNUSURU BWAWA LA MINDU


Baadhi wa watumishi wakionekana kukata majani yaliyochomoza kwenye Bwawa la Mindu
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiangalia mitambo ya kusafirisha maji iliyopo Tumbaku Morogoro 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiangalia mitambo ya kusafirisha maji iliyopo Tumbaku Morogoro 

Na Christina Cosmas,  Morogoro 

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kushirikiana na Bodi ya maji bonde la Wami Ruvu (WRBWB) kutimiza wajibu wao kwa  kuondoa majani  yaliyovamia Bwawa la Mindu ambalo ndio roho ya wanaMorogoro na kuliweka katika mazingira safi muda wote.

Waziri Aweso amesema hayo  akiwa kwenye ziara ya siku moja mkoa wa Morogoro kukagua bwawa la Mindu na mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji iliyopo mkoani hapa.

Waziri huyo alisema bwawa na mindu linapaswa kusimamiwa katika usafi ambapo bwawa hilo likitetereka litawaweka wakazi wa Morogoro katika hali ya kutojielewa.

Hata hivyo Waziri huyo aliwataka viongozi kushirikiana na kuhakikisha suala la uvamizi wa maeneo kwenye Bwawa hilo linapatiwa ufumbuzi kwa kuwapatia fidia zao walioingia kwenye maeneo ya Bwawa hilo mapema bila kusubiri wengine waingie na kuleta athari za zaidi.

"Athari za uharibifu wa vyanzo vya maji zinajulikana sasa tusiruhusu watu tena wakazidi kuongezeka, mkoa tukishikiana na Mamlaka mambo yatakwenda vizuri sana, lakini hili la fidia tuhakikishe kila anayestahili kupewa haki yake alipwe na lazima tulifanye kwa haraka ili kuanza kukabiliana na athari inayoweza kujitokeza" alisema Aweso.

Awali Mkurugenzi wa MORUWASA Mhandisi Tamim Katakweba alisema wameshakamilisha nyaraka za kazi ya kulinyanyua bwawa la mindu kwa ujazo wa mita 2.5 ili kukinga maji yanayomwagika kurudi baharini kwa zaidi ya miezi minne wakati wa kiangazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com